Mar 12, 2011
MAFUNZO YA WAELIMISHA RIKA KATIKA MASUALA YA UKIMWI MASHULENI
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Elimu rika kutoka shule za kata, kwa ujumla taarifa kutoka kwa watoto hawa wanayajua mengi na makubwa kuliko tunavyodhani!!!! wana maelezo ya kutisha juu ya uzoefu wao na ushiriki wao katika matendo hatarishi katika kusababisha maambukizi ya UKIMWI na magonjwa ya ngono
washiriki wakiwa wanapata chai katika mafunzo haya
Ninakumbuka kuwa mmoja alieleza namna wanavyotoa mimba katika shule yao: Kwamba kinywaji cha double punch hutumika kuharibu mimba kwa kunywa paketi mbili kwa mtu mwenye uja uzito!!!, Mwingine kuna mwanafuzi ametoa mimba vipande vikabaki mwilini, baada ya mwezi mmoja hali ikawa mbaya kizazi kikaoza na ameondolewa kizazi baada ya kushindikana.