Haki ya Mungu leo nimeshuhudia!!! Shirika la ADP Mbozi lilikuwa likizindua program yake ya uhakika wa chakula katika kaya kwenye kata ya Chitete wilayani Mbozi, ilipofika kwenye time ya chakula makundi yakatangazwa wageni wakale ukumbi huu na wengine mtapata chakula hapa hapa, kilichotokea watu walikuwa na mifuko ya rambo wameibana kwenye kwaba zao, mambo yakawa hivi!!!!!!!!!!!!!!!
Mama Nanihii unauweka, mwaga kwenye mfuko wangu kila mtu angalau sahani mbili kwanza!!!!! halafu naona hiyo sahani yako unajaza mno mbona mie unanitilia kidogo?
Huyu alipokuta sufuria halina kitu huku wenzake wakiendelea kujaza kwenye viroba hasira zikampanda akaamua kuanza kuangua kilio hadharani!!!!!!!!! waliiiiiiiii
Huyu akakumbuka kuwa hakuwa na mfuko wa rambo, lakini hawezi kosa ubwabwa wa kwenda nao nyumbani akaamua kujaza kwenye sahani huku baba kwa mbali akiwa amevalia T shirt ya chelsea akisogelea kunako ubwabwa!!