Adverts

Mar 18, 2011

MATUKIO YA PICHA KATIKA MUENDELEZO WA (MSIMU WA DHAHABU NA SERENGETI LAGER) KILIMANJARO KEMPINSKI.

Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dr. Emmanuel Nchimbi, akizungumza na wageni waalikwa wakati wa Uzinduzi wa Muendelezo wa Msimu wa Dhahabu na Bia ya Serengeti Lager, aliozinduliwa jana kwa vyombo vya habari kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam, ambapo wadau mbalimbali walihudhuria katika hafla hiyo kubwa jana jioni.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Bw. Richard Wells, akimkaribisha mgeni rasmi Dr. Emmanuel Nchimbi ambaye ni Waziri wa habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ili kuzungumza na wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo jana.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda, akikaribisha wageni mbalimbali katika hafla ya muendelezo wa Msimu wa Dhahabu na Serengeti lager, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski Jana jioni.
Mwanamuziki Gringo Junior wa Kalunde Band (katikati), akiwa sambamba na Wangenguaji wa bendi ya Kalunde Queen Vero (kulia) na Aminata, wakati wakifanya vitu vyao jukwaani wakati wa hafla hiyo.
Wanne Star na kundi lake wakawakilisha vyema muendelezo wa Msimu wa Dhahabu na Serengeti Lager kwa vivazai vyao vya Chuichui vinavyowakilisha Mnyama Chui kutoka mbuga za Serengeti..
Hizi zilikuwa pozi tu za Aminata (kulia)na Queen Vero wa Kalunde Band, kabla ya kupanda jukwaani.
Kutoka kulia ni wanamuziki wa bendi ya Kalunde Mwapwani, Sarafina na Remmy wakiimba katika hafla hiyo jana jioni.
Brand Manager wa Serengeti Lager Allan Chonjo, akiwa amepozi katika tuzo ya Dhahabu ya DLG ambayo bia hiyo imejishindia kwa mwaka huu wa 2011.
Waziri wa Habari , Vijana Utamaduni na Michezo Dr. Emmanuel Nchimbi, uso kwa uso na aliyekuwa msemaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Bw,Frolian Kaijage kama unavyowaona wakicheka sana, bila shaka kuna jambo limewafurahisha.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Angetile Osiah (kushoto), akiongea na Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Richard Wells, (katikati) ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni hiyo Teddy Mapunda.
Mkurugenzi wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)Richaed Wells, akiongea na Jan Paulsen Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, wakati wa hafla ya uzinduzi wa muendelezo wa Msimu wa Dhahabu na Serengeti Lager jana.
Wadau kutoka kampuni ya bia ya Serengeti kutoka kulia ni Warange, Bahari na Lutufyo.
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mh. Dr. Emmanuel Nchimbi, akitaniana na Mhariri mkuu wa Mawananchi Bw. Teophil Makunga, kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti jaji Marck Bomani na anayefuata ni Meneja wa Kinywaji cha Serengeti Lager Allan Chonjo. wa Kinywaji cha Serengeti Lager Allan Chonjo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Emmanuel Nchimbi wa pili kutoka kulia, akizungumza na Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Richard Wells, Wengine ni Mwenyekiti wa bodi kampuni ya Serengeti Jaji Marck Bomani na kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni hiyo Teddy Mapunda.
Wadau kutoka vyombo mbalimbali walihudhuria pia kutoka Sebo, Muyenjwa na Gerald.
Mwenyekiti wa Bodi kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Jaji Marck Bomani (kushoto), akifurahia jambo na Mwandishi mwanadamizi wa Gazeti la East African Joseph Mwamunyange katika hafla ya muendelezo wa Msimu wa Dhahabu na Serengeti Lager jana kwenye hoteli Kilimanjaro Kempinsk.
"