Mar 10, 2011
Mwakalebela Ashinda Tena Kesi Ya TAKUKURU
Mwakalebela wa pili kulia na mkeo Celina na ndugu wa wengine wa Mwakalebela wakitoka katika viunga vya mahakamani kwa furaha baada ya kuachiwa huru leo.
Aliyekuwa mshindi katika kura za maoni ndani ya CCM katika jimbo la Iringa mjini kupitia CCM Frederick Mwakalebela na mkewe Celina leo wameachiwa huru na mahakama ya hakimu makzi Iringa katika kesi yao ya rushwa katika mchakato wa kura za maoni baada ya mahakama hiyo kubaini kuwa hawana kesi ya kujibu.
Leo mahakama hiyo ilikuwa ikitoa maamuzi madogo ya kuendelea ama kutoendelea katika kesi hiyo ambayo ilifunguliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru ) mkoa wa Iringa.
Hii ni mara ya pili sasa Mwakalebela kuishinda Takukuru mahakamani hapo. Hivi karibuni Mahakama hiyo ilimwachia huru Mwakalebela kabla ya Takukuru kumfungulia tena kesi.
Hata hivyo wengi wamekuwa wakihoji sababu ya Takukuru Iringa kuendelea kung'ang'ania kesi hiyo huku watuhumiwa wengine wakiachiwa na mahakama bila kusumbuliwa kama ambavyo Mwakalebela anasumbuliwa na taasisi hiyo ya kuzuia na kupambana na rushwa kubwa na ndogo ndogo.. (Francis Godwin)"