Adverts

Mar 18, 2011

PROF.LIPUMBA AWASHUKURU WANACHAMA WAKE TANGA.,ACHUKIZWA NA UCHAKACHUAJI WA MATOKEO..

Mwenyekiti wa Taifa wa CUF Prof ,Ibrahim Lipumba akiwashukuru wana CUF waliojitokeza katika mapokezi yake leo,hapa ni nje ya ofisi ya wilaya ya CUF barabara ya 20 Wafuasi wa CUF wakimsikiliza mwenyekiti wao Taifa Prof Lipumba(hayupo pichani) Wazee wa CUF Tanga wakisalimiana na mwenyekiti wao Taifa Wafuasi wa CUF hapa wakiwa wamezuia basi la abiria kuendelea na safari baada ya kutaka kuharibu msafara wa mwenyekiti wao ,mapokezi haya yalikosa askari wa usalama barabarani wala ulinzi wowote wa polisi
WAFUASI wa chama cha wananchi (CUF) jiji la Tanga jana wamefunga barabara kuu ya kuingia mjini Tanga wakati wa mapokezi makubwa ya viongozi wa kitaifa wa chama hicho wakiongozwa na mwenyekiti wake Prof.Ibrahim Lipumba na katibu mkuu wake huku Prof Lipumba akishindwa kujizuia hisia zake na kuwa kesho atapasua jibu dhidi ya uchakachuaji wa matokeo ya uchaguzi mkuu mwaka 2010. Hata hivyo Prof .Lipumba kesho anakusudia kujibu tuhuma mbali mbali ambazo chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) wamekuwa wakizielekeza kwa chama hicho kuwa ni CCM 'B' na kuwa kimekuwa kikifanya kazi cha serikali ya CCM. Katika mapokezi hayo yaliyoanza umbali nje kidogo ya mji wa Tanga eneo la majani mapana viongozi hao walipokelewa na wafuasi wa chama hicho zaidi ya 2000 wakiwa na baiskeli ,pikipiki na magari huku baadhi yao wakitembea kwa miguu na kusababisha abiria waliokuwa wakisafiri na mabasi ya abiria kutoka jijini Tanga kwenda mkoani Dar es Salaam kusimama kwa muda kupisha msafara huo . Hata hivyo katika msafara huo ambao haukuwa na ulinzi wowote wa askari wa kikosi cha usalama barabara wala askari polisi ,wafuasi hao wa CUF walifanya kazi nzito ya kuwalinda viongozi hao wa kitaifa kwa kuzuia magari na baiskeli ambazo zilikuwa vikitaka kuchomekea msafara huo . Akizungumza na wananchi hao waliofika katika mapokezin hayo nje ya ofisi ya wilaya ya Tanga jiji Mwenyekiti huyo Prof.Lipumba mbali ya kuwapongeza kwa mapokezi makubwea bado alisema kuwa katika mkutano wake wa leo mchana utakaofanyika katika viwanja vya Tangamano jijini hapa . Prof.Lipumba alisema kuwa wananchi wa Tanga bado wanaimani kubwa na CUF na kuwa hata katkika uchaguzi mkuu uliopita wananchi hao walipiga kura za kutosha kwa chama hicho ila kura zao zilichakachuliwa na kuwataka wananchi kutokata tamaa kuendelea kujiunga na chama hicho . 'Ndugu zangu wanachana wenzangu wa CUF nawashukuru sana kwa mapokezi yenu makubwa mliyoyafanya leo....pia nawaukru kwa kura nyingi mlizozitoa kwa wagombea udiwani na wabunge pamoja na kura mlizo nipa mimi japo kura zilichakachuliwa ....nasema kesho katika mkutano wetu nitasema mengi kwa sasa niishie kusema ahsanteni sana' Prof.Lipumba katika ziara yake mkoani Tanga ziara yenye lengo la kuwapongeza wananchi kwa kura zao walizokipigia chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu,ameongozana na katibu mkuu wa chama hicho Taifa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga Amina Mohamed Mwidau. Kwa upande wake Mwidau pamoja na kuwapongeza wana CUF kwa mapokezi makubwa bado alieleza kusikitishwa na hatua ya jeshi la polisi kushindwa kutoa ulinzi katika mapokezi ya uongozi huo wa kitaifa na serikali . Hata hivyo mbunge huyo alisema katika kuwapongeza madiwani wa CUF waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana pamoja na kuwapongeza wana Tanga kwa kura zao walizotoa kwa wagombea wa CUF wanachama wote wanafanya mkesho kwa ajili ya kupongezana.
"