SERA YA VIJANA YA 2007
Mar 18, 2011
Sera ya vijana ya 2007 na utekelezaji wake
UTANGULIZI
Kuanzia uhuru 1961 kulikuwa hakuna sera yoyote ya vijana na maendeleo yao, zaidi ya kusema mambo yaliwahusu vijana na maendeleo yao yalitekelezwa kupitia sera zingine tu za maendeleo kama ushawishi kwa vijana na hasa kupitia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na chama tawala na serikali kwa upande mwingine. Lakini kwa sasa sera hii imezingatia kwa upande Fulani ibara katika katiba ya jamhuri ya muungano ya 1977 juu ya haki za binadamu yaani ibara ya 12 hadi 24.
ZANA YA VIJANA
Kijana ni kati ya miaka 15 mpaka 24 kwa mujibu wa umoja wa mataifa, na ni kati ya miaka 16 mpaka 29 kwa mujibu wa jumuiya ya madola, wakati kwa Tanzania ni 15- 35 kwa mujibu wa sera ya mwaka 2007 hapa ni katika maana ya kusema jamii inaamini anaweza kujishughulisha na kazi mbalimbali ikiwepo kupevuka na kujitambua.
IDADI / TAKWIMU
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 1995- vijana wa umri wa 15-24 ilikuwa ni asilimia 21% ya watanzania wote, wakati kati ya hao 49% ni wavulana na 51% ni wasichana na sehemu kubwa wakiishi vijijini ingawa kwa sasa kuna wimbi la wengi wao kwenda mijini (urbun centre)
SHUGHULI ZA KIUCHUMI
Imekuwa ikitegemea mazingira wanayoishi, umri, jinsia na rasilimali zilizopo kwa jumla. Lakini kwa jumla vijan wamekuwa wakijishughulisha na;
1. uzalishaji – kilimo, uvuvi, madini, na ufugaji.
2. biashara ndogo ndogo – uuzaji wa mitumba. Na takribani 3.4% utumishi wa uma.
NB:
Zaidi ya asilimia 60% ya wasionajira ni vijana na matokeo yake vibaka, wezi, na wakora, ni sehemu hiyo ya vijana wasionajira rasmi, na zaidi ya yote mijini imeonekana vijana wengi wamekuwa tegemezi kwa wazazi wao.
KIJAMII
1. Ukimwi - kiutafiti imeonekana wao ndio sehemu iliyoathirika zaidi hasa ukizingatia kuwa wamekuwa wakitumika zaidi kutokana makundi yote hasa (mafataki kiume na kike) kuwataka wao, na hasa ukizingatia ukata walionao kiraslimali.
2. ndoa – zaidi ya asilimia 60% ya zisizodumu ni katika kundi hilo la vijana.
3. madawa ya kulevya – hasa ukizingatia waswahili walisema mkono ukiuacha bila kazi basi hujitafutia wenyewe. Vivyo hivyo zaidi ya 60% ya vijana ni waathirika wa madawa haya. Kujitafutia kuvuta unga.
ELIMU
Elimu ya msingi ni takribani 400,000 lakini ni 10% hupata fursa ya kuendelea.
HAKI YA VIJANA
Haki ya vijana ni haki ya kitaifa.
UMUHIMU WA SERA YA VIJANA NA MAENDELEO YAO
Vijana ni nguvu kazi kubwa, kwani (60% ya work force) kwa nyanja zote yaani uzalishaji nk.
imeandaliwa na; M . S. MBUGI