Adverts

Mar 2, 2011

WANAFUNZI CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA MAGOGONI WACHANGIA DAMU KWA WAHANGA WA MABOMU.

Wanafunzi wa Chuo Cha Utumishi wa Umma Magogoni wakitoa damu kwa ajili ya kuchangia majeruhi waliojeruhiwa wakati wa milipuko ya mabomu katika kambi ya Jeshi la Wananchi JWTZ ya Gongolamboto iliyotokea hivi karibuni, katika picha kutoka kushoto ni Mariam Msabaha, Anet Kyaruzi na Sara Meena.
Peter Chami Mfayakazi wa Kitengo cha taifa cha Damu salama akimhudumia Mariam Msabaha mara baada ya kumaliza kutolewa damu wakati wanafunzi wa Chuo Cha Utumishi cha Magogoni walipotchangia damu kwa wahanga wa mabomu ya Gongolamboto chuoni hapo leo kulia ni Anet Kyaruzi.
Wanafunzi hawa wakisubiri kwenda kuchangia damu huku wakiwa na nyuso za furaha na matumaini kwa kuwa wanajua kwamba lengo lao ni kuwasaidia wenzao wenye matatizo kama ilivyo kwa wahanga wa mabomu wa Gongolamboto, Leo wanafunzi, waalimu na watumishi wengine wa chuo hicho wameamua kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia wahanga hao wa mabomu kutoka kulia ni wanafunzi Shakira Ismail,Glory Prosper na Neema Shabban.
"