Afadhali Tumepata Simu baada ya kutolewa Ethiopia.
Mfanyabiashara wa simu za mmkononi wa Kimataifa, Zahoro Matelephone (kulia) akimkabidhi nahodha wa timu ya Yanga kwa niaba ya wachezaji wote wa Yanga zawadi ya simu 30 za wachezaji baada ya kufanya vizuri kwenye mechi ya Ligi kuu dhidi ya watani wao wa jadi Simba
Mfanyabiashara wa Kimataifa wa Simu za Mkononi na mdau wa michezo nchini, Zahoro Hamisi ‘Matelephone ’ amewazawadia wachezaji wa timu ya Yanga simu 30 aina ya TINMO zenye thamani ya Shilingi milioni moja na nusu (1.5m) Dar es Salaam jana.
Akikabidhi zawadi hizo kwa nahodha wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa alisema yeye kama mpezi wa michezo na mshabiki wa Yanga alifurahishwa na kiwango kizuri walichoonyesha wachezaji hao wakati wa mechi ya Ligi Kuu Tanzaina Bara dhidi ya wapinzani wao wa jadi Simba.
Alisema Zahoro Matelephone ataendelea kufanya hivyo kila pindi timu hiyo itakapokuwa ikifanya vizuri ili kuleta hamasa kwa wachezaji kujituma zaidi.
Akishukuru zawadi hizo nahodha wa timu ya Yanga, Shadrack Nsajigwa alisema wao wanashukuru sana kwa kwa mdau wa soka na mpezi wa Yanga kuliona hilo na akatoa wito kuwa awape zawadi hata wanapofanya vizuri kwa timu zingine.
Alisema Nsajigwa hilo ni jambo zuri la kuigwa kwa wadau wengine wa michezo na mashabiki wa Yanga kufanya hivyo ili kuleta hamasa kwa wachezaji kucheza kwa kujituma zaidi.
Posted by Super D (Mnyamwezi) at 4:29 PM 0 comments
"