Adverts

Apr 24, 2011

BONANZA LA VETERAN MIKOA YA MBEYA NA NJORUMA YAFANA TUNDUMA

 Nyama Choma ilikuwepo na kila mchezaji alijichomea mwenyewe nyama yake, hapa ni mmoha wa wachezaji wa Mbozi Veteran almaarufu kama MWAJEKA HOTEL akichoma mshikaki katika bonanza kuubwa lililofanyika katika viwanja vya Chapwa jana jioni.Picha na Indaba Blogspot.com kwa ushirikiano na  blog dada ya Mbeyayetu.blogspot.com
Mfanya biashara maarufu katika eneo la TUNDUMA maarufu kama Brother K. Luhanga akiwa katika moja ya pilika za maandalizi ya bonanza hilo ambaye yeye pamoja na wadau wengine wameandaa bonanza hilo lililoshirikisha timu 10 kutoka wilaya za mikoa ya Njoruma na Mbeya.
 Mchezaji wa Yanga Fred Mbuna alikuwa kivutio katika bonanza hilo ambapo yeye pamoja na kaka yake  wa Tumbo moja Geofrey Mbuna walichezea timu ya Makambako Veteran ambapo waliifunga Tunduma veteran mabao 4-2 katika mchezo mkali uliofanyika jioni

POMBE NOMAAA!!! hapa watu waliendelea kulamba alamba alamba ya asili al-maarufu kama kikombe cha babu katika eneo maalumu lililoandaliwa kwaajili ya wadau wa hii kitu!


Timu ya VETERAN MAKAMBAKO ambapo Fred Mbuna wa kwanza waliochuchumaa mbele akiongoza timu yake kutoka na ushindi mnono dhidi ya Tunduma Veterean ambapo watu walifurahishwa na viwango vya timu hizo mbili zilivyocheza

Timu ya Veteran Njombe pia walishiriki katika mashindano hayo ambapo walitoka suluhu ya kutofungana na timu ya Veteran ya Mbeya katika mchezo ulifanyika saa 11.30 jioni



Jamaa akiwa ameshikiria pande la nyama ya kuku aliyechomwa katika viwanja vya Bonanza Chapwa ambapo kuku wa kienyeji walikuwa fwaaaaa!! na tamasha lilibeba ujumbe wa tumia fedha zikuzoeee, kujenga nyumba ni dalili ya woga wa maisha, kopa pesa halafu sepa/ingia mitini akikudai mpige chenga!!!! ilikuwa burudani tupu!!!!

Bi Mkubwa huyu al maarufu kama Mama Lao akimwaga ladhi kwenye moja ya shoo zake katika kufurahia bonanza hilo ambalo lilibeba watu wa aina mbalimbali katika viwanja vya Chapwa wilayani Mbozi. 


Mwandishi wa Blog hii Danny Tweve akifanya mahojiano na mchezaji wa timu ya Yanga  FRED MBUNA ambaye alichezea timu ya Makambako VETERAN na kuahidi kuipa kila msaada timu yake ya Makambako kutokana na kumjenga hadi kufikia kiwango cha sasa cha kuchezea timu ya taifa na Yanga!! walionyesha utulivu wa hali ya juu katika mchezo huo licha ya timu hiyo kuonyesha kuwa na wachezaji wengi waliowahi kushiriki katika michezo ya muungano pale Igowole.


Mkuu wa polisi Tunduma Sheikh Ally alikuwepo kwenye mchezo huo akiongoza timu ya Polisi ambayo ilitoka suruhu ya kutofungana na  timu ya Makambisee ya wabadilisha noti Tunduma, hapa yupo yeye na baadhi ya viongozi na wafadhiri wa timu za Tunduma VETERAN, MAKAMBISEE na Polisi Tunduma


Timu ya Makambisee ya wabadilisha fedha Tunduma wakiwa tayari kwaajili ya mchezo wao na timu ya Mbalizi Veteran katika mchezo uliokuwa mwishoni kabisa katika tamasha hilo ambalo halikuwa na wadhamini wa makampuni ya simu wala bia kama tulivyozoea jijini Dar es salaam na badala yake wafanyabiashara wa Tunduma walilibeba Tamasha zima kwa kugharimia baadhi ya Timu zilizoshiriki na kutoa burudani kubwaa. Big up  wafanyabiashara wa Tunduma

Hotel ya High Class  ya Tunduma ni miongoni wa wadau waliodhamini mashindano hayo yaliyovuta watu wengi wakiwemo majirani kutoka zambia, hapa gari la matangazo likiwa katika viwanja hivyo kuendelea kutoa burudani

Timu ya Veteran ya Mbozi ikiwa katika jogging kujiandaa na mechi hizo jana katika viwanja vya Chapwa ambapo Mbozi Veteran waliweza kuwaliza bao 1 kwa 0 Timu ya Veteran Tukuyu ambao waliongozwa na wachezaji kama Geofrey Katepa ambaye ameshachezea ligi kuu kwa timu za Tukuyu stars na  Tanzania Prisons

Pombe nomaaa kama kawaida vijana nao hawakukosekana katika kupata kikombe cha babu kwenye mazingira ya eneo la Bonanza ambapo waliendelea kulamba weeeeee mpaka jioni.

PICHA ZOTE NA DANNY TWEVE