Hatua hiyo inatokana na Mabonanza mawili yaliyofanyika miezi miwili mfululizo katika eneo la Mpakani mwa TANZANIA na ZAMBIA ambapo yaliendelea kuvutia timu nyingi kushiriki ambapo awali zilishiriki timu nne lakini sasa zimefikia timu 10 kutoka mikoa ya NJORUMA na Mbeya ambapo kwa Mkoa wa NJORUMA ulileta timu za Veteran kutoka Njombe na Makambako.
Mkoa wa Mbeya ulihusisha timu kutoka wilaya za Kyela, Mbeya Jiji, Rungwe, Mbeya vijijini, Mbozi na Tunduma ambayo ni wenyeji walioleta timu nne.
Licha ya baadhi ya makampuni ya simu kufika eneo hilo lakini walionekana kutoonyesha bidhaa zake kutokana na kutojitokeza katika udhamini huo ambao pia libeneke la http://www.dtwevetz.blogspot.com/ limekuwa mmoja wa wadau wanaodhamini mashindano hayo kwa kutoa ofa ya matangazo kwenye blog yake na kufuatilia shughuli nzima kila itakapofanyika.
Aidha Blog mama ya http://www.mbeyayetu.blogspot.com/ imekuwa mmoja wa wadau wanaofuatilia kwa karibu mashindano hayo ambayo katika mchezo utakaofuata yatahusisha pia timu kutoka nchi jirani ya ZAMBIA hatua ambayo pole pole yaanza kupandisha hadhi ya michezo ya timu ya veteran huku matamasha hayo yakitoa fulsa kwa familia kupata mahala pa kubadilishana mawazo na kujenga upendo, urafiki na udugu.
Wadau wa Bonanza wakishiriki katika nyama choma kama sehemu muhimu ya burudani katika michezo hiyo |
Kwa ujumla Bonanza hilo limeonekana kuongezeka mvuto kutoka tukio la kwanza ambapo tmu chache zilishiriki lakni sasa burudani imeendelea kupanda hadhi. Kulingana na taarifa zilizopatikana baada ya michezo hiyo ilielezwa kuwa maandalizi yanafanyika kufanya tamasha lingine katika mji wa Mbalizi mwezi May 20 mwaka huu na baadaye Makambako.
Hata hivyo wadau kutoka Tunduma wamesema wataendelea kuandaa matamasha mengine katika siku za usoni ambapo pia mashindano ya nyama choma, uchomaji wa samaki na upikaji wa chipsi yataaambatanishwa katika kushindanisha vijana ili kujua ubunifu wao katika shughuli hizo.
Mh Diwani wa Tunduma Frank Mwakajoka akisalimiana na wadau wa michezo waliofika uwanjani hapo kufuatilia michezo ya bonanza hilo |