Adverts

Apr 12, 2011

TAARIFA ZAIDI ZAZIDI KUZUA MASWALI JUU YA MZUNGU ALIYEFIA HOTELINI

Na Danny Tweve-Mbozi.

Taarifa za kifo cha mzungu kwenye hoteli ya Imperial Inn iliyopo Vwawa wilayani Mbozi zimezidi  kumiminika zikieleza kuwa kume kuwa na usimamizi mdogo kwa wageni wanaiongia nchini hasa kwenye miradi  mbalimbali hasa katika ufuatiliaji wa nyendo zao na matokeo yake kubeba kundi la watu wanaoacha madhara makubwa nchini baada ya mradi kumalizika.

Tukio la bwana Philip Halicon (28) raia wa Afrika kusini  aliyekuwa akifanya kazi kampuni ya Consolidated Construction Company (CCC) kumkuta mauti chumbani kwake akiwa na kete 8 za dawa zinazoaminika kuwa ni heroin na bangi gramu 3 ni dalili kuwa utaratibu huo upo pia kwa wageni wengine wanaotekeleza miradi kama hiyo.

aidha hofu ya wenzake kukataa asifanyiwe uchunguzi mwili wake, inadhihirisha kuwa ililenga kuficha ukweli juu ya kujihusisha huko na dawa za kulevya zoezi ambalo wamefanikiwa kulizima, kwani hadi mwili unaondolewa kwenye hospitali ya wilaya leo asubuhi, taarifa za ndani zinaonyesha kuwa haukufanyiwa uchunguzi.

Marehemu Philip Halicon alikuwa akiishi chumba namna 106 cha hoteli ya Imperial Inn iliyopo kando kando mwa barabara ya Mbeya -Tunduma eneo la Vwawa, lakini uongozi wa hoteli hiyo kupitia kwa meneja wake bwana Frederick Lupembe, amekuwa akitoa maelezo ya woga yanayoonyesha tayari keshazibwa mdomo asitoe ushirikiano kwa vyombo vya habari juu ya tukio hilo.

"Tayari idara za Usalama wa taifa na Polisi wanaendelea na uchunguzi wa suala hilo, hivyo taarifa zote zipo kwao nenda mkafuate huko, mimi hapa bosi mwenye hoteli amesema nisiseme kitu juu ya mzungu huyo aliyekufa" ndivyo alivyoeleza bwana Lupembe katika hali ya kuonyesha wazi hajui mwingiliano wa vyombo vya habari na idara alizozitaja.

Hata alipoulizwa kwani idara unazozitaja zinafanya kazi moja na vyombo vya habar? aliendelea kusisitiza nenda usalama wa taifa ama polisi".

Kwa ujumla taarifa za awali kutoka mazingira ya hoteli hiyo zinaonyesha kijana huyo alikuwa mtumiaji wa bidhaa hizo siku nyingi na kwamba kulikuwa na kitu kinaitwa "continous supply" ya mzigo huo dalili zinazojenga mashaka kuwa uchunguzi zaidi wa kiinteligensia unahitajika kufanyika kwa watumishi wageni wa makampuni haya ambao mwisho wa miradi hutuachia vichaa wengi kwenye maeneo yetu kutokana na kuwaonjesha vijana wanaofanya nao kazi.

Kampuni ya CCC inajenga barabara kuanzia Tunduma hadi Ikana na inaonyesha na Marehemu Philip alikuwa na madaraka ya Site Formen.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi  alipopigiwa simu na mtandao huu ametoa ushirikiano wa kutosha na kueleza kuwa kimsingi uchunguzi unaendelea juu ya kifo hicho na hasa katika eneo la vitu vilivyokutwa chumbani mwake, na kifo chake kwa ujumla.

Taarifa za tukio hilo zilibainishwa asubuhi ya Jumapili majira ya saa 1.30 wakati mzungu mwingine aliyekuwa akiishi hoteli ya jirani kumfuata bwana Philip kwaajili ya kumjulia hali na kisha waendelee na safari ya kuelea kwenye eneo la mradi ambapo Philip hakuonyesha dalili za kuamka hatua ambayo ililazimu uongozi wa hotel kwa pamoja kufungua mlango kuona kilichomsibu.
Mezani kwake vilikutwa vinywaji vikali pamoja na unga kete nane na bhangi gramu 3 ambavyo vilionyesha kuwa sehemu vimeshatumika katika usiku huo.

hata hivyo taarifa zaidi zinapasha kuwa mzungu huyo alikuwa akiumwa maralia na kwamba yawezekana alipuuza kuendelea na dozi kwa kuhofia kupoteza stimu ya unga na badala yake akaendelea kuji-kombelezea!!!



Baadhi ya maswali yaliyozuka kwenye mji wa Vwawa ni kuwa
  • Mzungu huyo amekuwa na mazoea ya kuingiza mabinti chumbani kwake kwaajili ya kufurahi maisha, je ni kwakiasi gani watanzania wenzetu wa kike wanaojenga mahusiano na wageni wamekuwakuwa wakiisadia serikali yao kupata taarifa za vitendo viovu ikiwemo matumizi ya unga yanayofanywa na wageni?.
  • Je wasichana waliokuwa na uhusiano na mzungu huyo wakamatwe na kueleza yaliyomsibu huyo mgeni?ingawa siku ya kifo inaelezwa kuwa mmoja aliyetaka kuja kujirusha naye alizuiwa kwakuwa afya ya jamaa huyo ilionekana siku hiyo kutokuwa nzuri.
  • Ni watanzania wangapi waliokuwa karibu na mzungu huyo walioshirikishwa kwenye ubwiaji wa unga kama sehemu ya kushare kama ilivyo kwenye sigara ambapo watu hugongeana? na ni mazezeta wanagapi tunawatarajia siku zijazo kutokana na madhara yaliyoenezwa na mzungu huyo?
  • Ni wazungu wangapi kwenye mradi huo wanaotumia unga kama alivyo kuwa huyo bwana na taarifa zao zinaripotiwa na kufanyiwa kazi?
  • Kwakuwa walilenga kukataa kufanya uchunguzi wa mwili wa marehemu je nini kilicho nyuma ya pazia miongoni mwao wazungu wenyewe?
  • Je mchana alikuwa hapati hiyo kitu unga akiwa kwenye kazi zake na gari alilokuwa analitumia dereva wake anajua nini juu ya bosi wake kutumia unga?
  • Huo mzigo unaingizwa wapi na unahifadhiwa wapi na unatumikaje na kwa kipindi gani stock inakwisha?
  • Je ni Unga na bhangi peke yake, wenye hoteli wanapofanya usafi kwenye vyumba vya wageni hawa wanaisaidiaje serikali kupata taarifa za ndani za kujitoshereza juu ya nyendo za wageni hawa?
MASWALI HAYA YA KIINTELIJENSIA YANAWEZA KUSAIDIA KUANZISHA KAZI KWA WATU KUFUATILIA NYENDO ZA WAGENI.
Wakati maswali hayo yakikosa majibu, Mwili wa marehemu Philip umesafirishwa kwa ndege kuelekea Dar ba baadaye Afrika kusini kukiwa na taarifa kuwa haukufanyiwa post moterm zaidi ya kuangalia tu.
Msafara wa mwili huo ulikuwa na ulinzi wa kujitoshereza kama kiongozi fulani, lakini hii yote ni katka kuthamini mtaalam wa kigeni ambaye alikuwa akitekeleza miradi ya maendeleo nchini.
TAARIFA ZINAZOZIDI KUINGIA KWENYE MTANDAO HUU JIONI....
Baadhi ya wahusika katika ufuatiliaji wa issue hii jioni hii wanakimbizana kuuzima mtandao huu  baada ya habari hii kumwagwa hadharani!!!
Habari zinazoingia sasa hivi kwenye mtandao zinaonyesha kuwa kuna watu wanahangaika kutaka kufuta maelezo yaliyomo kwenye blog hii kuwa "haikufanyika uchunguzi wa mwili wa marehemu -post mortem) na habari zaidi zinaeleza kuwa kuna dola za kimarekani zimesambaa mifukoni mwa watu jioni hii kutoka kwa wazungu wa mradi huo ili kuzima kelele za kufanyia uchunguzi mwili huo!!