Adverts

May 11, 2011

AJALI YA PIKI PIKI ILEJE YASABABISHA KIFO

Baadhi ya abiria wakimpa msaada wa majeruhi wa ajali ya piki piki ambaye aliburuzika na hatimaye kugongwa na gari la MSD  lilillokuwa likielekea wilayani Ileje akinyanyuliwa na wasamalia wema ili kuwahishwa hospitali
Dereva wa roli la MSD aliyevaa Dust coat akimbeba majeruhi baada ya gari lake kumgonga wakati akiviringika kwenda barabarani kufuatia kuanguka akiwa na piki piki katika kijiji cha IZUBA wilayani Ileje jana jioni. Dereva huyo wa piki piki amefariki mchana wa  leo akiwa katika matibabu kwenye hospitali ya wilaya ya Ileje na ametambuliwa kuwa alikuwa mfanyakazi wa kituo cha afya binafsi cha Sifika wilayani Mbozi.