Adverts

May 23, 2011

BONANZA LA VETERAN KILA MWISHO WA MWEZI LAENDELEA KUVUMA MBEYA

Kocha wa Timu ya Tunduma Veteran akitoa maelekezo katika kipindi cha pili wakati wakicheza na Mahasimu wao Makambisee ama wachenji dola wa Tunduma 

Kapten wa Timu  ya Makambisee Ayubu Sikagonamo akienda mapumziko baada ya kuongoza jahazi la timu hiyo hati halftime wakiwa nguvu sawa dhidi ya mahasimu wao Tunduma Veteran

Veteran Mbalizi wakiwa kwenye pozi la Picha, Katika michezo ya jana wao ndiyo walikuwa wenyeji wetu

Timu ya wenye mawe aka Fweza timu ya Mamilionaire ya MAKAMBISE Tunduma ama wachenji dola!!!

Wazee wa mujini Mbeya City Veteran wakiwa katika pozi la Picha wakati wakicheza na Tunduma Veteran ambapo waliambulia sare ya 1-1 dhidi ya Mbeya

Makambise Tunduma

Timu ya Veteran Mbozi wakiwa katika sura za bashasha kwenye mchezo kati yao na Mbeya jiji  ambapo walitoka nguvu sanwa kwa kufungana 1-1

Mwamuzi wa kike aliyechezesha mchezo kati ya Mbeya jiji na Mbozi  Atupakisye Jabir

Tunduma inajulikana kwa mambo yake hasa kwenye michezo ambapo vibweka na vituko ni sehemu ya michezo hapa shabiki mmoja alikuwa yeye ni kunywa kwa kwenda mbele

Add caption

Veteren Tunduma waliendelea kung'ara katika michezo yao yote baada ya mchezo wa awali kuwafunga MAKAMBISE 2-1 , mchezo uliofuata waliwalaza Mbalizi Veteran bao 4-0

Vipaji vya siku nyingi Makwaza ambaye alishachezea timu maarufu miaka hiyo mkoani Mbeya ya MECCO  akionyesha uwezo wake wa kugandisha mpira miguuni kwa muda mrefu

Mmoja wa mashabiki wa siku nyingi  ambaye kila mabonanza kama hayo yanapofanyika lazima ahudhulie yeye ni shabiki mkubwa wa timu ya veteran Tunduma(mwenye jinsi)