Adverts

May 19, 2011

BREACKING NEWS: MWENYEKITI HALMASHAURI RUNGWE AUWAWA KWA RISASI

MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe John Mwankenja ambaye ni diwani wa kata ya Kiwira ameuawawa kwa risasi usiku huu majira ya saa 5.00 wakati akishuka kwenye gari lake kuelekea nyumbani kwake.
Habari zilizoufikia mtandao huu zinaeleza kuwa alimiminiwa risasi kadhaa wakati akishusha mguu wake kutoka kwenye gari ili kuingia nyumbani kwake eneo la Kiwira.
Maiti yake inapelekwa hivi sasa hospitali ya Makandana kwa kuhifadhiwa, na hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo ambalo kwa ujumla linaaacha maswali mengi kwa wananchi wa wilaya ya Rungwe na mkoa  kwa ujumla.
Taarifa zaidi mtaletewa kadiri zitakapopatikana kutoka Rungwe