Adverts

May 6, 2011

CHADEMA WASABABISHA BARABARA MBEYA KUSIMAMA SHUGHULI KWA MUDA

 Haya ndiyo maandamano ya CHADEMA mkoani mbeya yakishirikisha wabunge karibu wote wa chama hicho pamoja na viongozi wao wakuu, hapa wakipita eneo la watu wengi la mwanjelwa kama mtandao wa  http://www.dtwevetz.blogspotcom/ ulivyonasa mchana huu 
 Magari ya viongozi wa CHADEMA yakiwa yanakwenda kwa mwendo wa harusi huku wafuasi wakitembea kwa mguu.Dr slaa naye aliamua kuongozana na Sugu kwa kutembea kwa mguu kutoka mwanjelwa hadi viwanja vya mama John kulikofanyika mkutano


Gari la hamasa likipita eneo laMwanjelwa huku likitoa burudani nakumbuka wimbo waliokuwa wakipiga una vijembe fulani kwa chama tawala.


Mbunge wa Mbozi Magharibi  David Silinde akipita eneo la Mwanjelwa katika msafara mreeefu wa viongozi wa chama hicho uliokuwa na mbwembwe za aina yake


Wazee wa vichupa , ama vikopo vya soda wakiwa katika gari lao tayari kwa lolote kama inavyojulikana kuwa wanaitwa Fanya lolote Uone!!!!!!!!!!!!!


Mafundi wa ujenzi wa soko la MWANJELWA badala ya kuendelea na kazi waliamua kushika viuno na kushangaa msafara unaopita barabarani wa wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA