Adverts

May 6, 2011

UJENZI WA SOKO LA MWANJELWA WAENDA VYEMA

KAMERAAAA KAMERA TUKAPIGE KAMERA................ ndivyo wanavyojadili mafundi hawa wakati mwandishi wa blog hii alipoitelekeza kamera yake na kuendelea kufuatilia picha za mnato wakati CHADEMA wanapita nje ya jengo la soko la Mwanjelwa leo jioni


Mama huyu ambaye ni miongoni mwa vibarua 300 wa mradi wa ujenzi wa soko la mwanjelwa akichungulia kwenye kamera ya mwandishi wa mtandao huu wakati akifanya kazi kwenye eneo la mradi ya kudocument.


Hili ndilo soko la MWANJELWA linavyoonekana katika ujenzi wake kwa juu , picha hii imepigwa mchana huu


Mwonekano wa soko la MWANJELWA kwa mbele


Soko linavyoonekana  kwa mbele


Site Manager -Mohamed Hasheed  akizungumza na blog hii kwenye mradi huo, kulingana na maelezo yake mradi huo umezingatia viwango vya kimataifa ikiwemo ujenzi wa barabara ya walemavu, vyoo vya walemavu, hifadhi ya maji ya lita 200,000 ambapo endapo maji yatakatika katika jiji la mbeya kwa zaidi ya wiki moja, hifadhi hiyo itaendelea kutoa huduma kwenye soko, wakati lita zinazobakia 50,000 zitahifadhiwa kwaajili ya majanga ya moto na itawekwa mashine ya kutambua hatari ya moto na kujiwasha kisha kuuzima.

General Formen wa mradi huo bwana Joseph Sebe akizungumza na indabaafrica blog katika mahojiano kwenye eneo la Mradi huo ambapo anaeleza kuwa soko litakuwa na jumla ya vyumba vya maduka 450, meza ndogo za bidhaa ngongo ndogo 480, kituo cha polisi, Majengo maalumu kwaaajili ya huduma za kibenki mawili na pia kutakuwa na jenereta la kutoshereza jengo lote.


Hii ndiyo sura ya soko hilo itakavyoonekana baada ya kukamilishwa ujenzi wake.


Mafundi wakiendelea na kazi za ujenzi wa soko la mwanjelwa ambalo itakumbukwa kuwa  ni matokeo ya kuungua kwa soko la awali ambali lilisabababisha wafanyabiashara wengi kupoteza mitaji yao mwaka 2006.