Adverts

May 14, 2011

ILEJE JIONI YA LEO IPO HIVI

Barabara inayoekelea Hospitali ya wilaya ikiwa imebakia kipande kidogo kutokana na kumeguka kwa mmomonyoko wa udongo, kwa ujumla katika maeneo mengi nimeshuhudia tatizo hilo  wilayani Ileje

Mto Mbimbi ambao umepita na kukitenganisha kijiji cha Itumba, unaonekana kingo zake kumomomonyoka ingawa ni mazingira yanayovutia

Kwa walioishi nchi za kusini mwa Africa mtakubaliana nami kuwa mmea huu unaheshimika sana hasa Swaziland unaitwa Umhlanga! ama kwa lugha yetu ni matete huu hutumika kumwonyesha binti yupi bikira kwenye sherehe za kimila za kila mwana anazozifanya mfalme Mswati. Inaelezwa kuwa kama binti siyo bikra akienda kukata mmea huu kwaajili ya kujenga uzio wa kutokea mfano basi ukatikaji wake hudhihirisha wazi kuwa amenanihii hivyo hapati nafasi ya matete yake kujenga ama kushiriki kwenye sherehe ile.

Ileje kuzuri bwanaa!