Adverts

May 26, 2011

,MAADHIMISHO YA SIKU YA KEMIA , TANZANIA YAFANA







Kakue Mafole kutoka ofisi ya mkemia mkuu wa Serikali (kulia) akiwaelezea waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) na waziri wa ofisi ya makamu wa Rais Mazingira Dk. Terezya Huvisa (wapili kushoto) jinsi ofisi hiyo inavyofanya kazi za kupima vitu mbalimbali. Waziri Prof. Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Picture no.2 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akimshauri Mkuu wa kitengo cha Kemia kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam Dk. Phillip Joseph jinsi gani wanaweza kufanya kazi ya kuchuja maji hadi kufikia hatua ya kuwa maji safi na salama kwa ufasaha zaidi na hivyo kuingia katika soko la ushindani wa biashara. Waziri Prof. Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia zilizoandaliwa na Chama cha wakemia Tanzania kwa kushirikiana na Kamisheni ya Taifa ya UNESCO uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Picture no.3 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akiangalia aina mbalimbali ya vitabu vya kufundishia somo la kemia wakati wa ufunguzi wa mwaka wa kimataifa wa kemia. Waziri Prof. Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe hizo zilizoandaliwa na Chama cha wakemia Tanzania kwa kushirikiana na Kamisheni ya Taifa ya UNESCO uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Picture no. 4 Brighton Jacob (wan ne kulia) mwanafunzi wa kidato cha nne kutoka shule ya Sekondari Kiluvya iliyopo jijini Dar es Salaam akimuelezea Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) jinsi ya kutambua aina mbalimbali za udongo. Waziri Prof. Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia zilizoandaliwa na Chama cha wakemia Tanzania kwa kushirikiana na Kamisheni ya Taifa ya UNESCO uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Picture no. 5 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akimsikiliza Sara Rubagumya (wa kwanza kulia) mwanafunzi wa kidato cha tatu kutoka shule ya Sekondari Tegeta iliyopo jijini Dar es Salaam kuhusu jinsi ya kuzalisha umeme kwa njia isiyo na gharama. Waziri Prof. Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Picture no. 6 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (watatu kutoka kushoto) akimsikiliza Salim Buyogera mwanafunzi wa kidato cha sita kutoka shule ya Sekondari Mbeta iliyopo jijini Mbeya alivyokuwa anaelezea jinsi vipande vya mabati vinavyoweza kuhifadhiwa na kutumika kufanya mambo mengine wakati wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Kushoto kwa waziri ni Naibu waziri wa wizara hiyo Philipo Mulugo na kulia kwa waziri ni Chande Othman mwenyekiti wa chama cha wakemia nchini.

Picha namba7 Elizabeth Mlay (kulia kwa waziri ) mwanafunzi wa kidato cha sita kutoka shule ya Sekondari Jangwani iliyopo jijini Dar es Salaam akimuelezea Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) jinsi ya kutengeneza dawa ya kusafishia na kuondoa harufu chooni. Waziri Prof. Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia zilizoandaliwa na Chama cha wakemia Tanzania kwa kushirikiana na Kamisheni ya Taifa ya UNESCO uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Picha na Anna Nkinda - Maelezo