Adverts

May 26, 2011

MAREHEMU FREDY KAOMBWE AAGWA, SALAM KUTOKA NJE YA NCHI NA NDANI ZAMIMINIKA

Ndugu zangu kwanza tupeane pole nyingi maana jambo hili limetushtua sana na hasa tunaomfahamu Fredi tangu tukuwa IRDP.

Nilibahatika kuhudhuria ibada ya kumuaga Fred iliyoongozwa na wachungaji 3 wa kanisa la anglikana Dodoma. Watumishi hawa katika sala zao, na hususan mahubiri wamejitahidi kutukumbusha kumtegemea Mungu kwa kila jambo na kuacha tamaa za kidunia.

Waombolezaji walikuwa ni wengi sana wakiongozwa na wakuu wa Wilaya za Bahi, Chamwino na Manispaa. Aidha mh.Mkuu wa mkoa wa Dodoma alihudhuria.

Mambo mengi sana yanasemwa kwamba inawezekana kajiua, au kauwawa. Hakuna hata mtu mmoja aliyejitokeza akasema ndiye alimpeleka hospitali kutoka eneo la tukio au ndiye aliyemjulisha marehemu kwamba mke wake alikuwa na hawara. Watu wa usalama watatusaidia ikifikia mahali pa kuchunguza kifo cha marehemu. Wengine wanasema hata simu yake haikupatikana.

Watu walihuzunika zaidi baada ya kusikia marehemu miezi 3 iliyopita amehitimu shahada ya pili katika fani ya maendeleo ya uchumi na biashara ya kimataifa huko korea ya kusini.

Fred amefariki akiwa na umri wa miaka 28 na ameacha mke na mtoto mmoja . Atazikwa Sikonge Tabora kesho. Msafara wa kuelekea Sikonge una watu wasiopungua 50-60 na tumeusindikiza hadi Nala (njia ya kuelekea singida saa 9.15 mchana.

Wale waliopo Tabora, hususan Wilaya ya Sikonge mtuwakilishe pia.

Tumwombe Mwenyenzi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.

Regards,

Nringi S.N.Urassa
BAHI-DODOMA.

TUNAOMBA WADAU  ANGALAU MUENDELEE KUTUHABARISHA  TUKIAMBATANISHA NA PICHA ZA MATUKIO HUSIKA ILI TUWE PAMOJA KATIKA SAFARI YA MWISHO YA NDUGU YETU FREDY KAOMBWE  HADI PUMZIKO LAKE LA MILELE! AMEN BY ANCHOR