Adverts

May 1, 2011

MWAKYEMBE AJA NA MAPENDEKEZO MAZITO YA KUBORESHA MIKATABA YA MIRADI YA BARABARA

 Naibu waziri wa Ujenzi amezungumzia mapendkezo kadhaa anayokusudia kuwasilisha kwa waziri wake JOHN POMBE MAGUFULI baada ya kutembelea miradi mbalimbali ya ujenzi ambapo
1. Anashauri miradi ya lami iongezwe kipindi cha matazamio kutoka mwaka mmoja hadi mitatu ili makampuni ya nje yabanwe kwakuwa yamekuwa yakitngeneza baadhi yabarabara katika kiwango cha chini na kuharibika mara baada ya kukabidhi.
2. Kushauri ufuatiliaji ama kuzuia fulsa za mikopo kwa makampuni yanayoomba advance na kuchelewesha kuanza mradi kwa kisingizio cha advance kutkutolewa huku yakitumia mikataba hiyo kwenda kupata mikopo benki hatua ambayo wanaelekeza mikopo hiyo kwenye miradi mingine nje ya ile wanayoisubilia advance payment.
3.Kupendekeza makampuni ya ndani yapewe sehemu za miradi mikubwa inayotekelezwa kwa fedha za serikali asilimia 100 badala ya kuendelea kuamini kuwa watanzania hawawezi kutekeleza miradi mikubwa ya lami, na kwamba kwa kampuni za ushauri wa miradi ya ujenzi anashauri zipewe kwa wingi kazi hizo kwakuwa hazihitaji mitaji mikubwa kama ilivyo kazi za ukandarasi kwenye miradi hiyo, anasema kwa sasa kuna makampuni 188 yaliyosajiliwa ya ushauri kwenye miradi hiyo lakini kati yake 133 ya kitanzania , hata hivyo ni kampuni moja ama mbili ndizo zilizopata kazi za maana.yeye anaona tunawachelewesha watanzania katika kukuza uwezo waona kuisaidia nchi.
4.Mameneja wa TANROADS mikoani wafuatilie na kuwalima barua makandarasi wa nje pale inapotokeza kushindwa kukamilishwa , ama kutofanya kwa ubora miradi yao ili fedha zingine zikatwe katika mikataba yao zikabidhiwe kwa mkandarasi atakayekamilisha kazi husika, na meneja ambaye atashindwa kusimamia wakandarasi hao katika eneo lake atawajibika mwenyewe kwa kusaidia kuiingiza serikali katika hassara.
5.Kufanya ufuatiliaji wa viwango vikubwa vinavyotozwa sasa nchini katika ujenzi wa barabara ya lami kwa kilometa ambavyo vimefikia bilion moja kiwango ambacho amesema,Tanzania isifanywe shamba la bibi na kwamba wanaenda kuyazungumza ili ikiwezekana kushusha viwango hivyo kwakuwa hakuna sababu ya msingi kwa lami hiyo hiyo nchi nyingine kutozwa chini ya kiwango cha Tanzania.akarejea kuwa miaka michache iliyopota bei ilikuwa milion 350 lakini imepanda ghafla bila sababu za msingi.
6.BOMOA BOMOA -ya makazi  ya wananchi ndani ya mita 30 kwenye eneo la hifadhi watalipwa ikiwa walijenga kabla ya sheria ya 2007 na kwamba wasibugudhiwe na kuwekewa alama za X kama ndiyo wakosefu, bali kuwepo na mazungumzo na kuelimishana kwakuwa serikali ndiyo inayohitaji kupanua barabara na siyo wananchi wameingilia barabara, vivyo hivyo kwa waliopitiwa na sheria ya awali ya eneo la hifadhi mita 22.5 pia ikiwa barabara hizo ziliwakuta wananchi basi wanapaswa kufidiwa.
8.Ujenzi unaoendelea barabara ya Namanga-Arusha (km 104) ujenzi wake unaendelea vizuri sana  na barabara hiyo inagharimu Bilion 81.77, Barabara ya kupitia makuyuni, Minjingu na Dodoma(barabara kuu ya capetown -misri), Minjingu-Babati inaendelea vyema, Dodoma kwenda Iringa Km259.8 tayari wameshaanza wakandarsi watatu na itagharimu Bilion 222.26 , Barabara ya Nzega hadi Tabora wataanza hivi karibuni ujenzi wake na itagharimu Bilion 129 kuijenga, Tabora kwenda Ulambo KM 94 itatumia bilion 111, Kwa ujumla miradi yotehiyo hakuna mradi unaotekelezwa na watanzania, hivyo anaenda kushawishi watanzania wawezeshwe.
Mkandarasi mpya amepatikana na anatekeleza barabara ya Mbeya -Lwanjilo  Km 36 ambayo itagharimu Bilion55  inajengwa na kampuni ya CCCC ya china    vivyo hivyo Lwanjilo-Chunya Km 36 kwa gharama ya Bilion40.3barabara hiyo ujenzi wake ulisimama baada ya mradi kumshinda mkandarasi wa awali
Dr  Mwakyembe akifafanua neno katika mkutano huo na wandishi wa habari.
Barabra ya Kintinku na Manyoni km 16 kilichojengwa na kampuni ya Tanzania ipo katika kiwango cha juu sana na imevutia kuanzisha hoja ya kuwapa fulsa watanzania.
Aidha alisema ameshuhudia udhaifu na ubovu wa barabara iliyojengwa kati ya Singida hadi Nzega umbali wa km 5(eneo la Shelui) ambayo sasa imeanza kukarabatiwa kwa fedha za ndani na kwamba kutokana na hali hiyo amemwagiza mtendaji wa TANROADS awasilishe taarifa ya kiufundi mezani kwake ili waitwe wote walioachia hali hiyo pamoja na mkandarasi mwenyewe wawajibike kwa hasara hizo.