Adverts

Jun 20, 2011

Filamu ya Safari ya Ikulu ya Maalim Seif yatia Fora ZIFF


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Maalim Seif Sharrif Hamad akiwahutubia wakazi wa Zanzibar waliofurika katika ukumbi wa Ngome Kongwe kushuhudia uzinduzi wa Filamu Maalum inayoelezea maisha yake ambayo ilionyeshwa kwa mara ya kwanza katika Tamasha la Filamu Zanziba linaloendelea hizi sasa kisiwani hapa.


FILAMU maalum iliyoelezea maisha na harakati za maisha ya mwanasiasa mkongwe, makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Maalim Seif Sharrif Hamad imezua gumzo kubwa baada ya kuonyeshwa kwa mara ya kwanza ndani ya tamasha la ZIFF.

Filamu hiyo ambayo ilibeba umati mkubwa wa wakazi wa Zanzibar ndani ya ukumbi wa Ngome kongwe ilipokuwa ikionyeshwa, wengi wa wakazi hao walionyesha kuipenda kutokana na mambo mbalimbali yaliyokuwemo katika filamu hiyo na hasa yale yaliyotokea kwenye uchaguzi wa Urais uliofanyika mwaka jana.

Baadhi ya matukio yaliyogusa hisia za wakazi hao ni pamoja na mikusanyiko ya wafuasi wengi wa chama cha wananchi, CUF, ambapo wananchi hao wengi wao walisikika wakisema kuwa waliibiwa kura zao.

“Hatukubali, kura nyingi zimeibiwa kumbe hali ilikuwa hivi nyuma ya pazia, hatukubali uchaguzi ujao tutafanya kila litakalowezekana” alisema Jamila Said, mkazi wa Chukwaani alieonekana katika filamu hiyo.

Kwa upande wake, Maalim Seif aliweza kuhutubia umati huo ambapo aliwasihi wananchi wa Zanzibar kufuata yale yote mazuri waliyoyashuhudia kwenye filamu hiyo ya maisha yake mpaka harakati zake za kuingia Ikulu.

“Jioni ya leo ni siku nzuri sana, nawapongeza waandaaji wa ZIFF na waliotengeneza filamu hii najua ilikuwa kazi kubwa sana, najua wengi mulikuw na shahuku ya kuona kilichokuwa nyuma ya maisha yangu hivyo nawaomba mukirudi muyashike yale yote mazuri kutoka kwangu” alisema Maalim Seif.

Pia aliendelea kusema kuwa, harakati zake hizo za siasa zilizodumu zaidi ya miaka 20 kwenye maswala ya harakati hizo za siasa za Tanzania na siasa za Zanzibar.

“Namshukuru mwandaaji wa filamu hii, Bw. Javed ambapo kwa mara ya kwanza aliponifuatailikuwa ni miezi mitano nyuma kabla ya uchaguzi.

Maalim Seif aliishukuru bodi ya ZIFF, kwa kuandaa tamasha hilo kila mwaka na kuiletea sifa Zanzibar kwani ulimwengu mzima unatambua umuhimu wa tamasha hilo. “Ni hakika ZIFF,imekuwa mlango wa maendeleo ya Zanzibar hivyo pongezi kwa uongozi wote wa ZIFF kwa kufanikisha hili’ alimalizia Maalim Seif.

Filamu hiyo imelikodiwa na kampuni ya ZG Films ya Zanzibar na iliweza kuonyeshwa kwa mara ya kwanza katika tamasha la ZIFF.
hii kutoka mtaa kwa mtaa blog
"