Adverts

Jun 20, 2011

Filamuya White & Black kugombea tuzo za Sembene ZIFF

Mkurugenzi Kiongozi wa Filamu ya White & Black kutoka Shirika la UNDER THE SAME SUN,Jean Francois (kushoto) akiongea na Waandishi wa Habari juu ya Filamu hiyo inayoelezea ukatili unaofanyika kwa watu wenye ulemavu wa ngozi nchini,katika ukumbi wa hoteli ya Seyyida Hotel,Zanzibar.Kulia ni Afisa Mipango wa Shirika la UNDER THE SAME SUN,Christopher Andendekisye na katikati ni Mtendaji wa Shirika hilo,Seif Kondo.
FILAMU iliyobeba ujumbe kuhusiana na unyanyasaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi nchini ya ‘WHITE & BLACK’ imeingia kwenye Tuzo ya Osmane Sembene, zinazotarajiwa kutolewa Juni 26 kwenye tamasha la Filamu za nchi za Majahazi maalufu kama ZIFF.
Akiongea na waandishi wa habari jana mjini hapa, Afisa Mipango wa shirika la Under the Same Sun, Christopher Andendekisye alisema kuwa filamu hiyo iliyotengenezwa kwa njia ya makala maalum iliyomhusisha mwandishi wa habari za uchunguzi nchini, Vicky Ntetema imeingia katika tuzo hizo na itaendelea kuonyeshwa sehemu mbali mbali ili kufikisha ujumbe kwa jamii nzima juu ya unyanyasaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi na ikiwezekana kukomesha kabisa ukatili huo utokanao na imani potofu.
Katika filamu hiyo, imeonyesa matukio halisi ya picha zilizotokea kwa walemavu hao huku kila mmoja aliyeshuhudia filamu hiyo wakiwemo waandishi wa habari walisisimka na kujawa na huzuni.
“Tanzania na sehemu nyingine za Afrika Mashariki, waganga wadanganyifu wamekuwa wakitumia viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi katika tiba zao, wakiamini kuwa viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi huleta bahati na mafanikio hii si kweli tunaomba wanahabari kufikisha ujumbe huu ilikokomesha kabisa” alisema Andendekisye.
Ndani ya filamu hiyo, Ntetema anaonekana kufatilia hatua moja baada ya nyingine kwa waganga wa kienyeji na sambamba na wauaji wa watu hao.
"