Adverts

Jun 7, 2011

UMISHUMTA MKOA WA MBEYA- KYELA YAWA KIDUME KWENYE SOKA

Afisa elimu wa wilaya ya Kyela akipokea kombe kutoka kwa kapten wa timu ya Wilaya hiyo baada ya kuwa mshindi wa jumla katika mchezo wa soka la wanaume katika michezo ya UMISHUMTA mkoa iliyofanyika katika kituo cha Iyunga sekondari.


Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Betha Swai akikabidhi kombe kwa Kapteni wa timu ya Kyela baada ya wilaya hiyo kuibuka kidume kwenye mashindano ya UMISHUMTA.

Kyela hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeendagha mwe eee jooo nyambala uju!!!!!! Jo Makyembe!!!!!!

Mshindi wa Riadha alikuwa Ileje - hawa walichukua pia kikombe baada ya kufukuza upepo kwa kiwango kikubwa na kutumia muda mfupi, milimani nako kunasaidia sana katika mashindano haya kuwa na pumzi!!

Chunya waliibuka mabingwa wa Mpira wa pete ama NETBAL katika mashindano hayo.

Dogo huyu aliibuka mkali wa somo la Historia, na mengine mengine  hapa akizawadiwa cheti

Dogo hapa mkali wa Namba - yeye hesabu na yeye, yeye na hesabu!! akizawadiwa cheti kutokana na kuwika katika mashindano ya taaluma mkoa wa Mbeya

Hii ndiyo timu ya Soka itakayowakilisha mkoa wa mbeya kwenye mashindano ya kanda yatakayofanyika Shule ya sekondari ya Kantalamba mkoani Rukwa kuanzia June 12 mwaka huu.

Wachezaji waliochaguliwa kuunda timu ya Mkoa wa Mbeya kwenye mashindano ya UMISHUTMTA yatakayofanyika kikanda mkoani Rukwa na baadaye kuunda timu ya kanda itakayoenda kupeperusha bendera huko Kibaha baada ya kumalizika kwa mashindano ya UMISETA.

Timu ya walemavu pia itashiriki katika mashindano haya, hapa ni baadhi ya wachezaji wa timu ya walemavu wanaoshiriki katika michezo ya riadha na michezo mingine.

Hapa ni timu zote zilizoshiriki mashidano hayo ya UMISHUMTA.


Timu ya walemavu kutoka shule ya msingi ya Itiji jijini Mbeya na Timu kutoka Katumba II  na Mwenge shule maalumu wilayani Mbozi wakiwa tayari kwa maandalizi ya kuunda timu ya kanda.

Afisa elimu mkoa Juma Kaponda akizungumza wakati wa ufungaji wa mashindano ya kimkoa.

Afisa elimu Mbeya Bwana Mapunda akiwa na afisa Michezo mkoa wa Mbeya bwana Mbijima katika uwanja ambako michezo ya UMISHUMTA  kimkoa imefanyika.
INDABA 2011