Adverts

Jul 6, 2011

NAPE AZIDI KUJENGA MAHUSIANO KATI YA CCM NA VYOMBO VYA HABARI


Katibu wa Nec, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akizungumza na viongozi wa magazeti ya kampuni ya Free Media Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, alipotembelea ofisi za magazeti hiyo mjini Dar es Salaam. 4/7/2007. Kulia ni Mhaririri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Absalom Kibanda
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akizungumza na Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Kampuni ya Free Media Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, Absalom Kibanda alipotembelea ofisi za magazeti hiyo mjini Dar es Salaam. 4/7/2007. Kushoto ni Naibu Mhariri Mtendaji wa kampuni hiyo, Asbert Ngurumo
Nape akiwa katika chumba cha habari cha gazeti la Tanzania Daima, alipotembelea ofisi za gazeti hilo 4/7/2011. Wapili kilia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free Media Ltd, Abnsalom Kibanda.
Nape akimsalimia mpigapicha mwandamizi wa kampuni ya Free Media. Francis Dande wakati wa ziara hiyo. Wapili kulia ni Mhariri Mtendaji wa kampuni hiyo Absalom Kibanda
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akiagana na Mhariri Mtendaji wa Free Media Ltd, Absalom Kibanda baada ya ziara katika ofisi za kampuni hiyo 4/7/2011. Katikati ni Naibu Mhariri Mtendaji wa kampuni hiyo Asbert Ngurumo.
Mwandishi wa Tanzania Daima Irene Mark akiwa kazini wakati wa ziara hiyo ya Nape
ZIARA YA NAPE MWANANCHI NA GLOBAL PUBLISHERS



Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye(kulia) akikumbatiana kwa fraha na Mhariri Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Daniel Msacky,alipotembelea ofisi za Mwananchi Communications Ltd, Tabata, Dar es Salaam, 29/6/2011. Kushoto ni Katibu Msaidizi Mkuu wa Itikadi na Uenezi CCM, Sixtus Mapunda.
Katibu wa NEC, Itikati na Uenezi, CCM, Nape Nnauye akizungumza na Wahariri wa magazeti ya Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, alipofaya ziara katika ofisi za kampuni hiyo, Tabata Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Sixtus Mapunda na Kshoto ni Mhariri Mtendaji wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Theophil Makunga, Mhariri Mrendaji gazeti la Mwananchi Dennis Msacky, na Mhariri wa Mwanaspoti Frank Sanga.
Waandishi wa habari wakiwa kazini katika chumba cha habari cha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti ya kampuni ya Mwananchi Communications Ltd.
Mhariri wa Habari wa Mwananchi, yahya Charahani akiwa kazini.
Mwandishi wa habari mkongwe wa Lauden Mwambona wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, akifurahi Nape alipoingia chumba cha habari cha magazeti ya kampuni hiyo.
Nape akionyeshwa maandalizi ya gazeti la Mwananchi katika hatua ya mwisho kabla ya kwenda kuchapwa mtamboni. Anayempa maelezo ni Makunga.
Meneja uzalishaji katika mtambo wa uchapaji magazeti ya kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Sameer Aher akimweleza Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye sehemu ya mtambo huo inavyofanya kazi.Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa MCL Theophil Makunga.
===================================================
NDANI YA GLOBAL PUBLISHERS
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisalimiana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Kiu, Ijumaa na Champion, Abdallah Mrisho, baada ya kuwasili Ofisi za kampuni hiyo, Mwenge, Dar es Salaam. leo . Wapili kulia ni Mhariri Kiongozi wa kampuni hiyo na Mhariri Kiongozi Oscar Ndauka na Mwandishi wa kampuni hiyo Luqman Maloto na wapili kushoto ni Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Sixtus Mapunda.
Nape akiwa katika ofisi za Global Publishers. Kushoto ni Abdallah Mrisho Wengine kutoka kulia ni, Sixtus Mapunda, Maloto,Ndauka na Mhariri kiongozi wa michezo wa Global Saleh Ally
Nape akizungumza na wafanyakazi wa Global Publishers katika chumba cha habari cha Global. Wengine ni Mrisho, Ndauka, Sixtus na Ally.
Waandishi wa habari wa kampuni ya Global Publishers wakiwa kazini wakati wa ziara hiyo ya Nape.
Kunfi la kwanza la wafanyakazi wa Global Publishers wakiwa katika picha ya pamoja na Nape baada ya kuzungumza nao leo
Kundi la pili la wafanyakazi wa Global Publishers wakiwa katika picha nya pamoja na Nape(picha zote na Bashir Nkoromo)


"