Adverts

Aug 28, 2011

DUNIA NI MFULULIZO WA MATUKIO! SIKU YAKIKUKUMBA BALAA!!!!!

Hapa ni majira ya saa 5 asubuhi nikiwa katikati ya mji wa Mbeya nikaona nisafishe sura ya gari kabla sijaondoka kwenda kijijini

Nikiwa milima ya senjele nikakumbana na tatizo, kumbe wakati wanaosha gari jamaa walifungua mfuniko wa rejeta kuchungulia maji, wakasahau kurejesha, nami nikaendesha bila kuangalia, gari likazima lenyewe, tukalazimika kuvuta umbali wa kilometa 40 hadi wilayani kwangu
Nafika Kijijini nakutana na jambo jipya kabisa, kijana wangu amelazwa hospitali ati kapata jeraha wakati wanajifunza sarakasi na wenzake, kitu chenye ncha kali kimemchana kwenye paji la uso!!! kwakweli akili ilisimama kwa dakika kadhaa kufikiri, mbona ni mfululizo wa matukio? nikagundua hii ni dunia, na ina mfululizo matukio

Kumbe wiki hii nikiimaliza salama, itakuwa kumbukumbu kubwa kwangu kwa  matukio ya mfulilizo matatu yenye afya!