Adverts

Aug 10, 2011

TIGO YAZINDUA BIMA KWA WATEJA WAKE

Baadhi ya maofisa wakionesha vipeperushi vya tigo bima watu wakijisajili na huduma hiyo ya tigo bima leo
wakimpatia mmoja ya wateja wao zawadi

Meneja Bidhaa, Joe Bendera (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na taratibu za kujiunga na Tigo Bima. Wahudhuriaji wengine ni Meneja wa Mitandao ya Tigo Ghana, Ferdinand Amenyah (kushoto) na Mratibu kutoka kampuni ya Microinsurance, Musa Lubango (kulia)
Watalaamu wa Tigo Bima wakionyesha vipeperushi vya Tigo Bima kwa waandishi wa habari
Nuru Salum (kushoto) mteja wa Tigo Bima akipokea zawadi kutoka kwa Meneja Bidhaa, Joe Bendera (kushoto), na katikati ni Mratibu kutoka kampuni ya Microinsurance, Musa Lubango (kushoto), Ferdinand Amenyah.
Mteja wa Tigo Bima (kushoto) akipewa maelekezo kutoka kwa wahudumu wa Tigo. Katikati ni Irene.
Meneja Bidhaa, Joe Bendera (kushoto) akielezea huduma ya Tigo Bima na mwandishi wa habari kutoka TBC 1, Lusanjo Mwakabuku. Tigo Tanzania wamezindua huduma ya bima ambayo itatoa faida kwa wateja wake kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, ikitwa Tigo Bima. Faida hii itagawiwa kwa wateja wa Tigo bure, wakitumia kiwango cha chini cha shilingi elfu tano kwa mwezi. Wateja wakulipa kabla wanaweza kujiunga na huduma hii katika vituo mbali mbali vya huduma kwa wateja hapa Dar Es Salaam. Kujiunga na huduma hii katika vituo hivi ilianza tarehe 27 Julai na ndani ya wiki mbili, wateja 1500 wameweza kujiunga na huduma ya Tigo Bima. Tigo Bima ni bima ya siku 30 ambayo imetolewa kwa wateja wa Tigo kuwalinda dhidi ya kupoteza maisha kutokana na ajali au ugonjwa. Inamlinda mteja na mmoja wa familia wa huyo mteja bure wakitumia shilingi elfu tano kwa mwezi mmoja, na ngazi ya bima hii inategemea na mteja anavyotumia huduma za Tigo kwa mwezi. Wakitumia Tigo zaidi wataweza kuongeza kiwango cha bima. Tigo Bima ni faida ya bure, ikimaanisha kwamba mteja au mmoja wa familia aliyechaguliwa akifariki, mrithi wake atapata msaada wa fedha wakati wanahiitaji bila kuwa na gharama yeyote kwao. Madai zitalipwa ndani ya masaa 72 baada yakupata nyaraka yanayotakiwa. Tigo imezindua faida hii mpya kwakushukuru wateja wake na kuwaonyesha kwamba Tigo inajali jamii. Tigo Bima inapatikana bure kwa wateja wa kabla wakijiunga na hivi karibuni itapatikana kwa wateja wakulipia badaaye. Bima hiyo inategemea na kiwango cha kiasi cha muda ya maongezi na Tigo. Bima yako inabadilika kila mwezi na kiwango cha bima yako inatokea na kile utakachotumia kwa mwezi iliyopita. Kama mteja anatumia shilingi 5,000 ndani ya mwezi wa kwanza bima yao itakuwa shilingi 200,000 mwezi inayofuata, ukitumia shilingi 10,000 -15,000 utapata bima ya shilingi 400,000, ukitumia shilingi 15,000 – 25,000 utapata bima ya shilingi 600,000, shilingi 25,000 – 40,000 utapata bima ya shilingi 800,000 na zaidi ya shilingi 40,000 utapata bima ya shilingi milioni moja mwezi inayofuata. Mwakilishi wa Tigo, Joe Bendera alisema “ Tunawahamsisha wateja wa Tigo kwenda kujiunga kwenye faida hii ya Tigo Bima. Hii ni faida yakusaidia wanafamilia na gharama ambazo wanakabiliana nazo wakimpoteza ndugu. Ili kuchukua fursa hii, wateja wetu wanatakiwa kwenda kujiunga na faida hii kwenye vituo vya huduma kwa wateja katika ofisi zetu Dar Es Salaam; Buguruni, mtaa wa Ghana, JM Mall ( Harbour View), Kariakoo, Mlimani City Mall na Nkrumah. Hivi karibuni tutaitoa faida hii katika mikoa mingine. Wakati wakujiunga, mteja anatakiwa kutoa jina lake, umri na namba ya simu na jina na umri wa ndugu yake ambayo amemchagua kumandikisha ka mrithi wake.” Tigo inatoa ufafanuzi juu ya ngazi za bima hii kupitia meseji fupi mwanzo wa kila mwezi kusudi mteja ajue amepata bima ya kiasi gani kwa mwezi iliyopita. Joe aliongezea” washindani wetu watajaribu kutufuata na faida hii ya Tigo Bima. Hata hivyo, tunatarajia kwamba Tigo itakuwa kampuni ya pekee ambayo itatoa huduma hii bure kwa wateja wao ambao watajiunga na Tigo Bima. Katika wiki mbili tangu kuzinduliwa kwake, Tigo Bima imepata majibu mazuri kutoka kwa wateja wao na tunaamini kwamba faida hii itapendwa sana, na kuwapa watu sababu yakutumia mtandao wetu.” Tigo Bima imeshirikiana na Golden Crescent , pamoja na Milvik na kampuni inayotoa huduma ya mafunzo na mtazamo wa utawala na kampuni hii inayoitwa MicroEnsure kuhakikisha utaratibu ya madai na kwamba mteja anapata malipo baada ya masaa 72.
SALAAM KWA TIGO} MUACHE KUTUNYIMA MATANGAZO WAKATI TUNAWATANGAZIA BURE KWENYE BLOG ZETU!!!
"