Adverts

Sep 20, 2011

Facebook Yampelekesha Jack ANUSURIKA KUVUNJIWA NDOA

Facebook Yampelekesha Jack

WANAUME wanaosaka wapenzi kwa njia ya mtandao wa kijamii, Facebook, wamemkong’ota staa wa filamu Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz ’(pichani). Kwa mujibu wa Jack, wanaume hao wamempa usumbufu mkubwa na kumsababishia matatizo kwa mpenzi wake. Kutokana na tatizo hilo, hivi karibuni Jack alifikia uamuzi wa kujitoa Facebook ili kunusuru uhusiano wake na mwenzi wake. Jack aliandika: “Naomba niwaage ya mwisho marafiki zangu, fans wangu, ndugu na wengine wote mnaonipenda nami nawapenda pia kutokana na mambo yaliyotokea kwa upande wangu siku ya leo ndo itakuwa mwisho kuonekana fb najitoa.” Alipozungumza na gazeti hili wiki iliyopita, Jack alisema: “Kuna watu wanaandika matusi kwenye ukurasa wangu, wengine wananiita mpenzi, hiyo inamuudhi mpenzi wangu. Wakati mwingine wanaandika meseji mbaya, kwa hiyo nimeona jambo la kufanya ni kujitoa,” alisema Jack. Hata hivyo, uchunguzi wa Uwazi umebaini kuwa Jack hajajitoa Facebook, badala yake ameendelea kutumbukiza vitu vipya, kuonesha kwamba dhamira yake ya mwanzo imefeli.