Adverts

Sep 20, 2011

THT Wahitimu

THT Wahitimu:
THT Wahitimu

KITUO cha Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT), kimewatunukia wahitimu wake 30 vyeti vya kumaliza masomo ya muziki katika mahafali ya sita yaliyofanyika eneo la Block 41, Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Katika mahafali hayo, wahitimu hao walipata nafasi ya kutoa burudani mbele ya wageni waalikwa na kukonga nyoyo za wengi.

Mbali na burudani ya wahitimu hao, wengine waliotumbuiza ni baadhi ya wasanii waliowahi kupitia THT, akiwamo Mwasiti Almasi, Elias Barnabas ‘Barnaba’, Lina Sanga ‘Lina’, Dotto Bernard ‘Dito’, Amini Mwinyimkuu ‘Amini’, Bernard Paul ‘Ben Paul’ na wengineo.

Baadhi ya wageni waliohudhuria mahafali hayo ni pamoja na wanamuziki Waziri Ally wa Kilimanjaro Band, Carola Kinasha, King Kiki, Abdul Salvador, John Kitime, Chai Jaba na Mkurugenzi wa African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka.

na Shabani Matutu

KUTOKA WAHAPAHAPA BLOG