Adverts

Sep 22, 2011

NAKONDE MPAKANI KWACHAFUKA, NI KUDAI MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS ZAMBIA


MICHAEL SATTA

Taarifa zilizotufikia punde zinasema hali ya mpaka wa kuingia zambia imekuwa chafu na serikali kulazimika kufunga mpaka, baada ya wafuasi wa kiongozi wa chama cha upinzani MICHAEL SATA kuanzisha vurugu kutokana na kucheleweshwa kutangazwa matokeo.

Mmoja wa vyanzo muhimu vya Indaba africa eneo la Mpakani hapo amedokeza kuwa kuna taarifa za kuchomwa gari moja la upande wa Tanzania ambalo inadaiwa limeunguzwa likiwa njiani kuingia nchini upande wa pili wa mpaka.
Inaelezwa kuwa wafuasi wa Sata wanaamini kuwa kiongozi wao ameongoza kwenye uchaguzi huo lakini serikali inachelewesha matokeo kwaajili ya kuyachakachua!.

Taarifa zaidi zinasema kutokana na hali hiyo magari mengi yaliyokuwa yamekamilisha taratibu kwaajili ya kuvuka mpaka yalilazimika kuegeshwa eneo la "No man's land" ili kuepuka uharibifu wa mali.

Joto la uchaguzi la Zambia limeendelea kupanda siku hadi siku kutokana na kiongozi aliyoko madarakani kudaiwa kutofautiana na kanisa katoliki nchini humo, hatua ambayo imempa nafasi kiongozi wa Upinzani SATA kuwa maarufu kutokana na kuungwa mkono pia na viongozi wa dini nchini humo.