Adverts

Oct 11, 2011

MABALOZI WATEMBELEA KABURI LA KARUME, NGORONGORO CRATER

Mabalozi wakiangalia meza ambayo ilivunjwa wakati akiuawa kwa risasi Rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume. (PICHA NA TAGIE MWAKAWAGO) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar, marehemu Abeid Amani Karume, eneo la Kisiwandui, Zanzibar. (PICHA NA TAGIE MWAKAWAGO) Kiongozi wa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini,Juma Mpango, akisoma dua kwenye kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume, mabalozi walipotembelea kaburi hilo mwanzoni mwa wiki.(PICHA NA TAGIE MWAKAWAGO) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini, pamoja na mtoto wa hayati Karume, Balozi Ali Karume (kulia waliokaa). Picha hiyo walipiga katika lango la kaburi la Karume, mjini Zanzibar.(PICHA NA TAGIE MWAKAWAGO) Mnyama kiboko akiwa kwenye maji wakati mabalozi wakitembelea Hifadhi ya Ngorongoro,mkoani Arusha. (PICHA NA ASSAH MWAMBENE)