Dandy Krazy al maarufu kama ZED |
na Danny Tweve -Lusaka
Mwanamziki Dandy Krazy wa nchini Zambia Maarufu kama ZED
ambaye hivi karibu wimbo wake wa Don’t kubeba(donch kubeba) ukimaanisha tunza
siri! Ameibuka akimtaka rais mpya Michael Sata ampe madaraka kwakuwa wimbo wake
ulifanya kampeni zilizomwezesha kuingia madarakani.
Akizungumza katika moja ya taarifa za Televisheni ya nchini
humo ya Muvi, Kratzy amesema wimbo huo ambao ulitumika kama slogan ya chama cha
Patriotic Front ulikuwa ujumbe mhimu katika mafanikio ya rais Sata baada ya
kutumika katika kipindi chote cha kampeni.
Mmoja wa wanaharakati nchini Zambia ambaye pia ni mwandishi
wa habari Henry Kabwe, serikali ya Zambia imelichukulia jambo hilo kama kitu
cha kawaida, ingawa mwanamziki huyo bado ameendelea kusisitiza kuwa anategemea
kudra za rais kumpa madaraka katika teuzi zake zinazoendelea.
ZED anatumia msemo huo ambao rais Satta alikuwa akisisitiza
wakati wa kampeni za kimya kimya kabla ya kutangaza nia yake ya kugombea urais
kwa mara ya kwanza baada ya kuacha kazi kwenye shirika la Reli la Uingereza .
Kutokana na madai hayo ya ZED wananchi wa Zambia wamekuwa
nyuma yake wakieleza kuwa mwanamziki huyo alijitoa moja kwamoja na kuonyesha
wazi kutunga nyimbo za kumpamba Sata na kwamba hatua yake ya kudai ujira wa
madaraka ni muhimu iungwe mkono
Staili ya wimbo huo inachezwa kama kiduku kwa mapaja
kutawanyika na baadaye kukutanishwa, imekuwa maarufu nchini Zambia na wimbo huo
umekuwa ukipigwa kwenye maduka ya kanda
na yale ya kawaida licha ya kampeni na uchaguzi kwisha.
Donch kubeba imemfanya ZED kuwa adui wa chama cha MMD ambacho
kilikuwa kimemsimamisha mgombea wake kwa mara ya pili Rupia Banda.
Kwa ujumla mali zilizokuwa zikimilikiwa na chama hicho
ambazo zilitokana na michango ya wananchi zimenyang’anywa na serikali ya sata
ikiwa ni pamoja na michango iliyokuwa ikichukuliwa kwenye masoko na ushuru
mwingine.