Adverts

Nov 20, 2011

JK AELEKEA DODOMA KUKUTANA NA WABUNGE WA CCM, KAMATI KUU NA NEC

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete (kulia), akisalimiana na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango wakati wa hafla hiyo. (PICHA ZOTE NA IKULU)

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete (kulia), akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, John Shibuda (CHADEMA), alipokutana naye kwenye Uwanja wa Ndege wa Dodoma. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Pius Msekwa.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete (katikati) akizungumza na baadhi ya wabunge wa chama hicho, kwenye Ukumbi wa St Gasper, mjini Dodoma

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete (kulia), akisalimiana na baadhi ya wabunge pamoja na viongozi wa chama hicho, alipowasili katika mkutano na viongozi hao katika Ukumbi wa St. Gasper, mjini Dodoma jana, ambapo aliwataka kwenda kwenye majimbo yao kuwaeleza wananchi kuhusu mchakato wa Mswada wa Katiba Mpya.

Spika wa Bunge, Anne Makinda (kulia) akiteta jambo na Mbunge wa Viti Maalum, Margareth Sitta (CCM) katika hafla hiyo.