Adverts

Nov 26, 2011

Maazimio Ya Kikao Cha NEC Ya CCM Haya Hapa

Wilson C. Mukama KATIBU MKUU WA CCM akiongea na waandishi wa habari,
--
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi iliyokutana kwa siku mbili kuanzia tarehe 23-24 Novemba, 2011 mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mambo mengine imeazimia yafuatayo:
UNUNUZI WA MAHINDI I. Halmashauri Kuu ya Taifa imeipongeza Serikali kwa kuwa na mkakati wa kutafuta fedha haraka kwa kuamua kuuza mahindi tani 80,000 kwa UNFP na nchini Kenya ili kwanza, kulipa madeni ya wakulima, na pili, kununua mahindi ya wakulima yaliyopo majumbani na kwenye vituo vya ununuzi kabla ya upandaji wa msimu mpya haujaanza. II. Imeipongeza pia Serikali kwa kuruhusu uuzaji wa mahindi nje ya nchi, hali ambayo itasaidia mahindi yaliyobaki kwa wakulima kupata soko. Hata hivyo, imesisitiza kuwepo na tahadhari sasa na siku zijazo, ili chakula chote kisiuzwe nje ya nchi na kusababisha tatizo la njaa nchini.Kwa