Mkuu wa chuo cha Mipango Dodoma-Constantine Lifurilo amezungumza na wanachuo wapya wapatao 2400 akielezea matarajio makubwa katika kusambaa kwa taaluma ya mipango katika ngazi mbalimbali za jamii.
Akizungumza kwenye baraza hilo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, amesema kada ya mipango itaendelea kulaumiwa ikiwa watalaamu wake watashindwa kukidhi matarajio ya wananchi kwakuwa nafasi zao zinaweza kupoteza mwelekeo wa jamii ikiwa watatumia vibaya nafasi hizo kwakuwa program zote za maendeleo duniani kote zinahusisha watalaamu wa maendeleo katika kuandaa misingi ya kupanga,kuweka mwelekeo na hatimaye katika kutekeleza.
Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi wa Chuo anayeshughulikia -Mafunzo Profesa Innocent Zilihona amesema, chuo hakitawavumilia watu watakaobadili chuo hicho kuwa chuo cha sanaa, kutokana na kuvaa mavazi yasiyo na staha kwani kufanya hivyo kutakuwa ni kudhalilisha fani ya mipango ambayo kwa sehemu kubwa chuo hicho ndicho kilichopewa jukumu na taifa kuandaa wataalamu na viongozi wa baadaye.
Amesema ni vyema wanachuo wakatambua kuwa chuo hicho kina "core values" zake ambazo zimewekwa kutokana na dhima ambayo serikali imekipa chuo hicho kuandaa viongozi, hivyo kuruhusu watu kuachia miili yao nje ni kupoteza misingi ambayo imekijenga na kukikuza chuo hadi kufikia hatua ya kupokea wanachuo 2400 na kwamba ili kuona kuwa misingi haipotoshwi, kitahakikisha wasiyofuata maadili wanarejea kwao.
Naye Mkurugenzi Msaidizi katika eneo la Utawala na Fedha Tibelio Mdendemi amesema, ni vyema fulsa ya mafunzo ya vitendo na nadharia inayotolewa na chuo ikatumiwa vyema na wanachuo katika kujiandaa kutumikia taifa kwani, ni aibu kwa wao kushindwa kutekeleza majukumu yao wawapo kazini wakati chuo kimewezesha maandalizi yao kwa kiwango cha juu.
Ametaja kuwa miongoni mwa changamoto za sasa kwa vyuo vingi nchini ni kutoa wahitimu ambao tabia zao, mwenendo na madaraka wanayoenda kushika havifanana hali ambayo amesema, kwa chuo cha mipango kitahakikisha kinalisimamia suala hilo na kuhakikisha kinatoa wataalamu bora na wenye nidhamu na kuthamini majukumu wanayoyatumikia.
|
Baadhi ya wanachuo waliohudhulia Baraza la kwanza jana katika ukumbi wa Nyerere |
|
Msajiri wa wanafunzi Katikati bwana Titus Mwageni pamoja na Waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi kushoto na kulia kwake ni Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho |
|
Maprofesa na Madaktari wa wahadhiri wa chuo cha Mipango wakifuatilia kwa makini taarifa na hotuba zilizotolewa jana |
|
Mkurugenzi wa Chuo cha Mipango Constantine Lifurilo kushoto akiwa na msaidizi wake katika masuala ya Utawala na Fedha Tiberio Mdendemi |
|
Rais wa serikali ya wanafunzi Bwana Haule akizungumza kwenye Mkutano huo |
|
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Tiberio Mdendemi akizungumza katika baraza hilo ambapo alieleza wazi kuwa chuo cha Mipango ni tofauti sana na vyuo vingine, hivyo masuala ya mavazi na udhadhifu ni sehemu muhimu ya mafunzo kwa wanachuo wake kwakuwa wanaandaliwa kuwa viongozi! |
|
Mkurugenzi wa Chuo cha Mipango Dodoma- Constantine Lifurilo akizungumza na wanachuo wa kozi za astashahada, stashahada, shahada na stashahada ya uzamili katika mipango ya mazingira, Maendeleo vijijini, Mikoa, Idadi ya watu, Miradi ,Utawala bora na maendeleo endelevu pamoja na Uwekezaji |
|
Taa haiwekwi uvunguni ili kumilika bali huwekwa juu " ni maneno ya Profesa Innocent Zilihona Makamu Mkuu wa chuo cha Mipango eneo la Mafunzo akizungumza na wanachuo |
|
Serikali ya wanachuo wa chuo cha Mipango Dodoma |
|
Rais wa serikali ya wanafunzi |
|
Mdendemi " wanaoachia nywele ovyo ovyo kama wendawazimu hapa hatuwahitaji, masuala ya kuvalia suruali makalioni hapa kwishineaaa!!!! |
|
Profesa Katega wa kwanza kushoto akifuatilia mjadala pamoja na wahadhiri madaktari wanaoongoza idara mbalimbali chuoni hapo |
|
Darasa la POST GRADUATE wakiwa katika majadiliano |
|
Kiti kinachoonyesha mamlaka ya chuo cha Mipango Dodoma ambacho hukaliwa na Mkuu wa chuo, Mwenyekiti wa Bodi ama kiongozi anayealikwa kufanya jukumu fulani kwaniaba ya Bodi na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. |