| Taarifa zilizotufikia hivi sasa ni kwamba Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro
amekatisha ziara yake wilayani Mbozi na alikuwa njiani kurudi jijini Mbeya kukutana
 na wamachinga waliouteka mji tangu asubuhi. Kinachosubiriwa ni iwapo wamachinga
 hao watakubali kuongea naye kwani walishatamka kuwa hawataki kumuona.
Muda huu machinga walikuwa wakilazimisha kuingia katikati ya jiji kushinikiza
 kuachiwa kwa wenzao wanaoshikiliwa na polisi |