Adverts

Nov 12, 2011

SIKU YA 12 YA NOVEMBRE.....("SAMEDI") NANYI MSALIPO, SALINI HIVI........

Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe Hapa duniani kama mbinguni Utupe leo riziki yetu, Utusamehe deni zetu Kama sisi nasi tuwasemehevyo wadeni wetu Na usitutie majribuni, lakini utuokoe na yule muovu Kwakuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele.
Amina.
Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao Na Baba yenu wa mbinguni, atawasamehe nyinyi Bali msipowasamehe watu makosa yao Wala baba yenu hatawasamehe nyinyi makosa yenu
MATHAYO 6:7-14
Hii sala imejitosheleza na imebeba kila kitu Huna haja ya kujielezea maneno meeeeeeengi Kuorodhesha mipango ya miaka 10 ijayo Ukisema tu hii, Mungu anakuwa anajua hitaji la kila mtu katika moyo wake Atakutimizia kadri unavyopaswa kupewa Sabato Njema