Adverts

Nov 20, 2011

Wasia mfupi wa Prof.Ali Mazrui

Prof.Ali Mazrui ni msomi , mwandisi, mwalimu na nyota ya Afrika . Alizaliwa February 24, 1933 huko Mombasa Kenya. Alipata degree yake ya kwanza kwa kufaulu vizuri sana huko Manchester Uingereza baada ya kushindwa kufanikiwa kuingia chuo cha Makerere Uganda.

Alijaribu mara kadhaa kwani hakufanya vizuri mtihani wake wa sekondari kwa wakati ule lakini hakukata tamaa hatimaye alifanikiwa kuendelea na masomo Uingereza.

Baadaye alichukua shahada yake ya uzamili (Masters) katika chuo kikuu cha Columbia New York. Na baadaye shahada ya udaktari kutoka chuo kikuu cha Oxford Uingereza. Kusoma zaidi bofya

Alifanya kazi kwa miaka 10 mkatika chuo kikuu cha Makerere Uganda chuo alichoshindwa kuingia kama mwanafunzi lakini alirudi kama shujaa na mwalimu aliyekuwa amejaa sifa tele.

Alifanya kazi pia katika chuo kikuu cha Ann Arbor Michigan (1978-1991) kama mkurugenzi wa kitengo cha masomo ya Afrika na wamarekani weusi.

Pia amekuwa akilakwa kutembelea vyu mbali mbali katika nchi mbali mbali ikiwa ni pamoja na Singapore, Australia,Malaysia, cairo, Nairobi, Tehran,Uingereza, Baghdad n.k.

Pia amefanya kazi kwa miaka minne kama rais wa jumuiya ya waislam wanasayansi jamii wa Marekani? (Washingtion Dc).

Mwakaq 2005 Jarida la Marekani la sera za mambo ya nje (Washington Dc) na lile la Uingereza lilimteuwa Ali Mazrui kuwa mmoja wa wasomi 100 wa hali ya juu walio hai.

Ameandika zaidi ya vitabu 30 ikiwa nin pamoja na Towards a Pax Africana ?(1967) na The political sociology of the English language (1975)akiielezea Sociologia ya lugha ya kiingereza.

Mambo mengi aliyozungumzia ni pamoja na siasa za Afrika , utamaduni wa kisiasa wa kimataifa , siasa za kiislam na uhusiano wa kusini na kaskazini.

Dr. Mazrui pia ameandikia magazeti kjama London Times,New York Times,Sunday Nation (Nairobi), Al-Ahram (Cairo), The Guardian (London) na Lagos,The Economist(London) and The Cumhuriyet(Istanbul na Ankara) , Yomiuri Shimbun (Tokyo na Osaka), Int.Herald Tribune (Paris), Elsevier (Amsterdam), Los Angeles Times(USA), The Starndard Nairobi Afrique 2000 (Brussels and Paris), City Press (Johanesburg) na Monitor-Kampala.