Adverts

Jan 11, 2012

GARI YA KAMPUNI YA ULINZI YABAMBWA NA VIPODOZI MBEYA, NI G4S, POLIS NAO WAKAMATWA

GARI ya Kampuni ya Ulinzi binafsi ya G4S iliyokuwa ikitokea mji mdogo wa Tunduma, wilaya mpya ya Momba mkoani Mbeya imekamatwa na Mamlaka ya mapato nchini (TRA) Mkoa wa Mbeya, ikiwa na bidhaa haramu(vipodozi).
Taarifa za uchunguzi zimebaini kuwa tukio hilo lilitokea Januari 6, mwaka huu majira ya saa Nane mchana ambapo gari hilo lililofukuziwa na Maafisa wa TRA kisha kulikamata eneo la Songwe, wilaya ya Mbeya vijijini.
Baada ya ukamatwa gari hilo na kuvikamata vipondozi hivyo na wanawake wawili ambao ni wamiliki wa vipodozi huku wakiwemo Askari wawili wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya na Askali wengine wa kampuni hiyo ya ulinzi.
Gari hilo lenye namba za usajili T.690 AMA aina ya Toyota Landcruiser baada ya kukamatwa lilipelekwa katika ofisi za Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA), mkoa wa Mbeya.
Kwa upande wake Meneja wa TRA mkoani hapa Anord Maimu, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo licha ya kuwa nje ya ofisi kikazi na kwamba suala hilo ameliachia Jeshi la Polisi mkoani hapa.
Maimu amesema Mamlaka ya mapato nchini kwa mkoa wa Mbeya imeteketeza vipodozi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 129, vilivyokamatwa kwa kipindi cha mwaka uliopita.
Ametoa onyo kwa wananchi wanaojihusisha na biashara hiyo haramu kuacha mara moja, kutokana na utumiaji wa vipodozi hivyo kuathiri afya hali ambayo husababisha ugonjwa wa Kansa.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi amekiri kupokea taarifa hizo kutoka kwa Meneja wa TRA mkoani hapa na kwamba Askari wake waliohusika na usafirishaji wa bidhaa hizo haramu wakibainika na tukio hilo watachukuliwa hatua za kijeshi. kutoka mbeya yetu