Kampuni kubwa zinazoendesha huduma za mitandao ya internet za Google na Wikipedia zimeaza leo kufanya mgomo wa kuishinikiza serekali kuzuwia muswada mpya ambao unatarajiwa kusomwa mwenzi Februari kwa ajili ya kudhibidi upatikanaji habari zinazopitia kwenye mitandao mbali mbali ya internet.
Miswada hiyo kulingana na kauli ya mkurugeni wa Wikipedia Jimmy Wales unaonyesha dhairi kabisa utaweka vikwanzo vikubwa sana kwa upatikanaji wa habari au usambazaji wa habari na utuaji huduma wa mitandao mbali mbali ya internet kwa watu duniani kote zikiwemo nchi masikini.
Miswada hiyo miwili inayojulikana kama SOPA (Stop Online Piracy Act) na PIPA (Protect IP Act) ndio miswada ambayo inapingwa na makampuni ya makubwa yanayotoa huduma za habari kupitia mtandao wa internet.
Kupitiswa kwa miswda hiyo kunaweza kusababisha watu wa nchi masikini hata nchi zilizo endelea kutopata habari mbali mbali kutokana na uhuru wa habari kudhibitiwa na kusababisha huduma mbalimbali zinazotolewa na makampuni makubwa kama GOOGLE ambayo hutoa huduma kama za blogs kupitia blogger.com kuwalazimu kuthibiti kila kinachoingizwa kupitia huduma blogs suala mbalo ni gumu sana na litateta athari za upatikanaji wa habari kupitia mitandao.
Miswada hiyo itakapopitishwa itawalazimu Google kuchuja habari ambazo zinaingizwa kupitia blogs zote, kutokana na sheria mpya. Pia upatikanaji habari kwa nchi masikini utakuwa hafifu kwa sababu wale wote wanaoendesha mitandao ambayo si mikubwa, kama vile blogs na website ambazo zinajiendesha kimasikini na malipo ya kima cha chini hazitoweza kuonekana tena kwenye mitandao ya Google.