KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA BW THOBIAS ANDENGENYE AKIZIPANGA RISASI
AMBAZO ZILITUMIKA KATIKA TUKIO LA KUUA ASKARI KATIKA ENEO LA SHANGARAI
KATIKA hali isioyokuwa ya kawaida askari polisi F 228 Constebo Kijanda Mwandru amefariki dunia, pamoja na mkuu wa upelezi wilaya Faustine Mwafele kujeruliwa vibaya na jambazi sugu mkoani hapa ambaye amejulikana kwa jina la Hendry Samson Kaunda. Akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa mapema leo kamanda wa polisi mkoa wa arusha Andengenye Thobias alisema kuwa tukio hilo lilitokea leo majira ya saakumi za alfajiri.
Kamanda Andengenye alisema kuwa katika tukio hilo lilitokea mara baada ya askari hao kwe nda kwa ajili ya upekuzi katika nyumba ya Bi Agness Silas ambayo ilikuwa ikitumika kwa ajili ya makazui ya majambazi mjini hapa. Alibainisha kuwa mara baada ya askari hao kufika katika eneo la tukio kwa bahati mbaya jambazi hendry aliwavamia askari hao na kisha kuwapiga kwa risasi mfulululizo hali ambayo ilimsabbishia kifo askari huyo pamoja na kumjerui Mrakibu huyo wa wilaya ya Arusha vijijini.
Pia alisema kuwa mara baada ya kutokea kwa tukio hilo polisi waliendelea na msako mkali katika nyumba hiyo ya Bi Agness ambayo ilikuwa inasadikiwa kuwaficha na kuwatunza majambazi na kisha kukuta vifaa mbalimbali ambavyo vilikuwa vinatumika kwa ajili ya shuguli za ujambazi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Alitaja Vifaa hivyo kuwa ni pamoja na risasi 36,risasi 12 aina ya Short gun ,kitako kimoja cha bunduki aina ya Shortgun,pamoja na soksi za kuvaa usoni ambazo walikuwa wakizitumia majambazi hayo katika shuguli mbalimbali za uhalifu.
Bw Andengenye alieleza kuwa katika tukio hilo watoto wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa upelelezi zaidi ambapo watoto hao ni DainessMsawe(9) pamoja na Alex Paramina (13) ambaye ndiye aliyefumfungulia mlango Jambazi aliyeuwa na kujerui askari polisi. Aidha mrakibu wa jeshi la polisi bado anaendelea na matibabu katika hospitali ya Selian wakati polisi ikiendelea na msako dhidi ya majmbazi hayo yaliyokimbia.