Mithali19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; bali mke mwenye busaramtu hupewa na Bwana”. Ni matumainiyangu kwamba u-mzima kijana mwenzangu na una maendeleo mazuri kiroho nakimwili. Katika waraka huu mfupi kwa vijana nataka kujibu swali hili ambalovijana wengi wamekuwa wakijiuliza. Wengine kutokana na kutojua ukweli wakewamejikuta wakifanya maamuzi ambayo hadi leo wanayajutia . Kibiblia,tunajua kabisa ni mpango wa Mungu tuweze kuoa au kuolewa. Sasa swali linakuja,je ni lazima Mungu anionyeshe, anipe mke au mume wa maisha yangu? Kwani mimikijana sina uwezo wa kuangalia mtu kisha nikaomba Mungu na mwishonikajichagulia mwenyewe? Au kifupi maamuzi ya nani atakua mume/mke wangu ni yanani? Hili niswali ambalo vijana wengi limekuwa likiwachanganya. Wengine wanaamini maamuzihayo ni ya Mungu kunipa mke/mume na wengine wanaamini Mungu hahusiki, bali waondio wenye nafasi na wanaohusika. Sasa hayo ni mawazo yao wala mimi sitakikuyapinga lakini ngoja nikuonyeshe Biblia inasema nini halafu utajua ukweli niupi:- Kwenyekitabu cha Mithali 19:14 , Mungu anasema suala la nyumba, mashamba, maduka navyote vifafanavyo na hivi nimewapa uwezo na ruhusa wazazi wako baba & mama)wa mwili wakupe lakini suala la mke au mume mwenye busara mimi pekee ndiyeninaye wajibika kukupa .Sikiliza kama unataka mke/mume kwa ajili ya kulitumikiakusudi la Mungu alilokuumbia basi huna budi ni lazima upige goti kuomba nakisha ungoje Mungu akuonyeshe/ akupe mke/mume wa kusudi lake. Vijana wengiwanafikiri eti kwa sababu wameokoka, na wamejzwa roho mtakatifu basi wanao –uwezo wa kujichagulia mke/mume wa kuishi nao. Sikiliza kama una amini umeumbwakwa kusudi la Mungu na unataka kutembea katika njia yake basi mruhusu Munguakupe mke/mume mwenye busara ya kukaa na wewe. Mke au mumeana sehemu kubwa katika maisha yako. Anaweza akabadilisha maisha yako, yakiroho, kiuchumi, kimwili, kihuduma na kima husiano na watu wengine.Hivyokibiblia maamuzi ya nani atakuwa mkeo au mumeo ni ya Mungu na si ya kwako. Hiiina maana ukimuomba Mungu hakika atakuletea mtu halisi wa kukaa na wewe. Lakinimaamuzi ya kumkubali au kumkataa ni ya kwako na si ya Mungu. Ukikubali shaurila Bwana litatumikiwa, ukimkataa, umejikaribishia laana. Zifuatazo nisababu za msingi zinazomfanya Mungu akuchagulie/akupe mke/mume na siokukuruhusu wewe/wazazi/ukoo wako/mchungaji wako kukuchagulia mke. (a)Kusudi la uumbaji (kuwaunganisha). Sikiliza hakuna mtu aliyeumbwa kwa bahati mbaya, Mungu ndiyo aliyekuchagua nasiyo wewe uliyemchagua na akakuweka duniani ili umtumikie sasa yeye ndiyeanayejua nikimuunganisha huyu kaka na yule dada watalitumikia kusudilangu. Warumi 8:28-29. Mungu anapofanya maamuzi anafanya kwakuangalia kusudi lake na muda na wahusika wa hilo kusudi. Yeye ni Mungu naanafanya kwa utikufu jifunze kuruhusu mapenzi ya Mungu yatimie na si ya kwako. (b) Mungu ndiye ana-fahamu nani mwenyebusara ya kukaa na wewe. Mithali 19:14b Busara ni uwezo uliomo ndani ya mtu (mke/mume) unaomsaidiakujizuia kufanya jambo ambalo liko nje ya mpango/mapenzi ya Mungu kwa kufanyalile lilio katika mapenzi ya Mungu.Hivyo Mungu pekee ndiye anaye mjua mke/mumemwenye busara ya kukaa na wewe, kamwe wewe hutaweza mjua bila uongozi wa Mungu. (c) Sababu za ki-Agano. Zaburi: 32:8 Siku uliyofanya maamuzi ya kuokoka maana yake uliyakabidhimaisha yako kwa Yesu, ukamwambia nafungua moyo wangu uingie uyatawale nakuyaongoza maisha yangu sasa hilo ni Agano lako kwa Mungu. Kwa sababu hiyo Yesuanawajibika kwako kukufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea, hii ikiwa nipamoja na kukupa mke/mume wa kukufaa. (d)Mawazo yake, si mawazo yako. Isaya 55:8 Sikiliza Mungu anayo mawazo (mipango) na njia (mikakati) yakukufanikisha kimaisha. Sasa katika kutekeleza mipango yake kwako na kupitiawewe lazima atumie mikakati yake ili kutekeleza mawazo yake. Sasa moja yamikakati yake ni kukupa mke au mume wa kusudi lake . Sasa, sikatai huenda kwa jinsi ya mwili ni kweli huyo mtu anayekupa Mungu anaupungufu fulani. Huenda umbile lake, sura yake, kabila lake, rangi yake,dhehebu lake, haliko kama ulivyo kuwa unavyotaka wewe. Mungu anakupa mke au mume kutokana nasababu hizo ambazo nimekuekezea hapo juu na ninakuhakikishia ukimkubali atakupaneema ya kukaa naye huyo mtu na kukufanya uridhike naye na kumpenda huyomwenzako .
Nakutakia uongozi wa Mungu katika eneo lamaamuzi ya nani atakua mumeo au mkeo .