KATIBU MKUU wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr.Wilbroad Slaa amemtangaza Boid Mwabulanga kuwa katibu wa chama hicho mkoa wa Mbeya na kumweka kando Eddo Makatta Mwamalala.
Hali hiyo ilijitokeza jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Nzovwe na kushangaza wanachama wengi ambao walikuwa hawajui mvutano uliopo kati ya Dr. Slaa na Mwamalala tangu mwaka 2010 katika uchaguzi Mkuu.
Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya chama hicho zimeeleza kuwa Mwamalala alivuliwa ukatibu tangu mwaka jana katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Mbeya Peack Hotel uliopo Jijini Mbeya na baada ya kuona hivyo alisafiri na kwenda Jijini Dar es Salaam kuomba huruma ya Dr.Slaa lakini alikataliwa hata kuonana nae.