Na, Mwanafasihi Wetu,Brantyre-Malawi
LIPO jamboambalo limegubika utata nchini Malawi juu ya Dkt. Hasting Kamuzu Banda halisianayedaiwa kupotelea nchi za Ughaibuni na baadaye kupachikwa Dkt. Kamuzu Banda wabandia ili kuficha jambo ambalo hadi sasa Wamalawi wenyewe wanatafakari juu yautata huo.
Taarifa zauchokonozi kutoka nchini humo zinadai kuwa utata huo uliibuka mara baada yawananchi wazalenda wa Malawi kuhitaji kuwaondoa watu weupe kwa kilekilichoonekana kuwepo na unyanyasaji dhidi yao ambapo aliibuka mwanaharakatiJohn Chilembwe aliyejitoa mhanga kuwakomboa Wamalawi.
Chilembweambaye hadi sasa anaenziwa kwa picha yake kukaa katika noti za nchi hiyoanadaiwa kluanzisha harakati za ukombozi ambazo hatimaye zilisababisha kuteswa,kufungwa na kuuawa kikatili na serikali ya kikoloni.
Kifo chaChilembwe ndicho kilichoibua hoja ya kuwepo mabadiliko na kuhitaji kuwaondoawalowezi weusi waliojikita nchini Malawi ambayo awali ilikuwa ikiitwa SouthernRhodesia ambapo katika harakati hizo waliibuka Madaktari wawili ambaoi ni Dkt.Hasting Kamuzu Banda(Mwafrika) na Dkt. Richard John Amstro (mzungu)ambaowalikuwa nje ya nchi ya Malawi miaka ya thelathini wakifanya kazi ya Udaktari.
Imedaiwakuwa madaktari hawa wawili waliishi na kufanya kazi pamoja huku Dkt.Amstroakiwa amepangwa na wazungu kurithi nafasi ya kuongoza Malawi mara baada ya kutimuliwakwa wazungu akiuvaa U-Kamuzu Banda badala ya Dkt. Kamuzu Banda halisi.
Kwa mujibuwa uchokonozi kutoka katika vyanzo mbalimbali ndani na nje ya Malawi zinadaikuwa kilichofanyika ni kumpika Dkt. Amstro kwa kukariri tabia na mila zaWamalawi akitumia fursa ya ukaribu wake na Dkt. Kamuzu Banda halisi ambapo piainadaiwa alijaribu hata kuijua familia ya Kamuzu iliyopo katika kijiji chaKasungu nchini Malawi.
Inaelezwakuwa wakiwa huko ughaibuni ndugu wa familia ya Dkt. Kamuzu halisi hawakujuakinachoendelea bali kutokana na maslahi ya nchi za Magharibi ambazo kwa wakatihuo hazikuhitajika kuishi nchini Malawi ilitumika mbinu ya kumpoteza KamuzuBanda halisi na badala yake kupandikizwa Kamuzu Banda feki(Dkt. Amstro)aliyerejea nchini Malawi na kujiita Dkt. Hasting Kamuzu Banda.
Hadi sasahakuna anayejua alipo Kamuzu Banda halisi huku kukiwa na madai ya kuuawa nakupotezwa kaburi lake ambapo kwa mujibu wa watoa taarifa ni kwamba tarehehalisi ya kuzaliwa Banda(halisi) ilikuwa ni mwaka 1889 na Kamuzu Banda fekiDkt. (Amstro) alizaliwa 1901.
Inaelezwakuwa Dkt. Banda halisi alienda kusomea Udaktari nchini Uingereza mwaka 1934 nabaadaye alikwenda nchini USA ambako alipata PHD na ndiko huko alikokutana naDkt. Kamuzu Banda feki Dkt. (Amstro).
Dkt. Amstroalirejea Malawi akiwa kama Dkt. Hasting Kamuzu Banda na kwenda moja kwa mojakijijini alikozaliwa Dkt. Banda halisi ambap[o hata hivyo wanafamilia wa Dkt.Banda hawakuridhika na nasabu yake kutokana na maumbile yao kwa kuwa Dkt. Bandahalisi alielezwa kuwa alikuwa na vidole vine katika mguu wake wa kushoto hukuDkt. Amstro akiwa na kilema hali ambayo ilikuwa ni tofauti baina ya watuiwawili hao.
Noto za Malawi zenye picha ya John Chilembwe |
Dkt. Hasting Kamuzu Banda anayedaiwa kuwa ni Mzungu |
Hata hivyojitihada za kidiplomasia zilifanyika hadi wanafamilia hao wakakubali kuwa nindugu yao ingawa hawakuridhika ambapo alijitahidi kupeleka huduma nyingi zakijamii katika mji huo wa Kasungu na kufanya wakazi wa eneo hilo wasahau kuhojinasabu ya Dkt. Amstro na hivyo kulazimika kumkubali kuwa ndiye Dkt. KamuzuBanda.
Katikauongozi wake Dkt. Banda aliwaweka karibu watu kama akina John Tembo ambapobaadaye lilizuka kundi la watu waliohoji uhalisi wa Dkt.Hasting Kamuzu Bandakama vile Mwandishi wa vitabu Kanyama Chiume, Dunduzu Chisisa, Gwebe,Chiwanga,Olton Chirwa, Mtangazaji Denis Liwewe, Kamungu, Aron Gadama, Chiwanga nawengine wengi waslioamua kuikimbia nchi hiyo.
Inaelezwakuwa baadhi ya watu waliokuwa wakifuatilia sakata hilo kama vile Gadama naChiwanga walitengenezewa ajali katika barabara ya Tsisangani ambako walipotezamaisha, na kuwa mpango huo ulikuwa chini ya kikundi maalumu cha Kimafiakinachofahamika kama Malawi Young Pioneer ambacho kinadaiwa kuwa ni hatarikuliko hata jeshi la Malawi.
Hata hivyokatika utawala wa Dkt. Kamuzu Banda aliyeingia kwa ajili ya kulinda maslahi yaWazungu akijifanya ni Mmalawi na President wa Muyaya aliweza kuboresha hali yawakulima wa nchi hiyo kiasi cha kuwasahaulisha machungu waliyokuwa nayoWamalawi juu ya historia ya kuingia kwake madarakani.
Dkt. Bandaaliishi na kupewa mke ambaye inaelezwa hakubahatika kuzaa naye na aliyekuwaKatibu Muhtasi wake aliyefahamika kwa jina la Cesilia Kazamila.
Dkt. Bandaalifia nchini Afrika Kusini alikoenda kwa ajili ya matibabu mwaka 1997 wakatinchi yake ikiwa ndani ya mageuzi chini ya utawala wa chama kingine cha UDFkilichoongozwa na mwenyeji wa Mangochi mwenye asili ya Uyao Alhaj Bakili Muluziambapo baadaye Rais Bingu wa Mutharika ndiye aliyechukua nafasi hiyo hadi sasa.
Nchi ya Malawiimepata Uhuru wake kutoka kwa Waingereza mwaka 1964 ikiwa ni miaka mitatu baadaya Uhuru wa Tanganyika.
Katikakuenzi harakati za ukombozi za nchi hiyo baadhi ya wasanii wa nchi hiyowametengeneza igizo maarufu linalozungumzia John Chilembwe ambaye ndiyeanayeelezwa kuwa ni mkombozi wa kweli huku baadhi ya waimbaji wakiimba nyimbombalimbali za kuomboleza vifo vya wanaharakati waliotengenezewa ajali naserikali ya wakati wa Dkt. Kamuzu Banda.
Aidhavuguvugu la mageuzi wakati wa ukoloni nchini Malawi linaelezwa kuwakimbiza raiawengi wakiwemo Rais wa Kwanza wa Visiwa vya Zanzibar Abeid Aman Karume,akinaOscar Kambona,John Chipaka na wengine wengi waliohama nchi hiyo kwa sababuzinazoelezwa kuwa ni ukandamizaji wa wakoloni.
kutoka fasihi za ufasaha blog