Wafanyakzi wa Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania, wanaotoa huduma mbalimbali katika kambi za waathirika wa mafuriko jijini Dar es Salaam wakiandaa ugali wa mchana hii leo katika eneo la Mabwe Pande nje Kidogo ya jiji la Dar es Salaam ambako baadhi ya waathirika hao wanaandaliwa viwanja na makazi ya muda.
hapa ni ugali unaonjwa kama upo tayari kwa kuliwa.
kazi kubwa wanayo ifanya Msalaba Mwekundi hapo Mabwe pande hivi sasa ni kujenga makazi ya Muda ambayo waathirika wa mafuriko hasa wale waliokuwa na nyumba mabondeni watahamia.
mahema yaliyo kamilika yaliwekwa nembo maalum za Shirika hilo.
Mslaba Mwenkendu imetoa mahema zaidi ya 200 katika eneo hilo ambayo tayari yamefungwa.
Hakika eneo hili litakuwa zuri na lililo katika mpangilio mzuri sana pindi wahusika wakifika na kujenga makazi yao ya kudumu. Seruikali imeahidi kusogeza huduma zote muhimu kama maji, Umeme na vituo vya afya katika eneo hilo. Lakini watu wanahofu juu ya waliokuwa wamiliki wa nyumba hizo za jangwani na bonde la Msimbazi kuwa kama wataenda kuishi huko. Ama watauza viwanja hivyo?
kutoka father kidevu