Adverts

Aug 9, 2012

ROLI LASHINDWA KUPANDA MLIMA NA KUFUNGA BARABARA MBOZI

Kreti za soda zikiwa zimemwagika barabarani  baada ya kupinduka kwa roli mali ya Kanji lanji ambalo lilikuwa limebeba creti 1800

Hilo ndilo roli lililokata njia  likionekana kwa mbali

Huu ndiyo msururu wa magari kwa upande mmoja wa barabara

BIBI HUYU AKIWA KWENYE FOLENI YA KUCHUKUA SODA


ABIRIA WANAOTUMIA BARABARA YA MBEYA –TUNDUMA LEO WAMEONJA ADHA YA BARABARANI BAADA YA GARI LA MIZIGO LILILOBEBA MASANDUKU YA SODA KUPINDUKA NA KUFUNGA BARABARA HADI  JIONI HII .
GARI HILO LENYE NAMBA ZA  USAJI T 788 AEY MALI YA KAMPUNI YA KANJI LALJI YA MBEYA, LILIKUWA LIKIPELEKA SODA MKOANI RUKWA AMBAPO KUTOKANA NA UZITO WA MZIGO LILIOBEBA LILISHINDWA KUPANDA MLIMA WA SENJELE NA DEREVA KUAMUA KUOKOA UHAI WAKE KWA KUKATA NJIA.

BAADA YA TUKIO HILO ABIRIA WALIOKUWA KWENYE MABASI YANAYOTUMIA BARABARA HIYO WAKAFANYA SHEREHE YA KUNYWA NA KUSAZAA SODA HIZO BILA KUJALI TAHADHARI ILIYOKUWA IKITOLEWA NA MMOJA WA WAHUSIKA KWENYE ROLI HILO ALIYEJITAMBULISHA KAMA DEREVA WA GARI LILIPATA AJALI PETER NAMLAZAR

HATA HIVYO WATU WALIENDELEA KUCHANGAMKIA SODA HIZO LICHA YA ULINZI WA POLISI KUWEPO ENEO HILO.

LICHA YA KUTOKUTOKEA MAAFA YEYOTE KWA WALIO KUWEMO KWENYE GARI HILO, UNYWAJI OVYO WA SODA ZILIZOANGUKA ENEO HILO LIMETAJWA KUWA NI HATARI KWA MAISHA HASA KUTOKANA NA VIPANDE VYA CHUPA KUCHANGANYIKA NA SODA HIZO