Mratibu wa sensa wilaya ya Mbozi Eliud Mwakibombaki akizungumza kwenye uzinduzi huo |
Baashi ya watu waliohudhulia uzinduzi huo |
Mzee Mdalavuma akifuatiwa na Mkuu wa wilaya wakiwa meza kuu |
Dr Michael Kadeghe Mkuu wa wilaya ya Mbozi akiwahamasisha wananchi kushiriki kwenye zoezi la sensa |
Kikundi cha Ngoma cha Ndili miongoni mwa vikundi vilivyoshiriki kwenye zoezi la uzinduzi wa kampeni ya hamasa ya sensa jioni ya leo uwanja wa kituo cha mabasi cha Mlowo |
Na Danny Tweve
BAADHI YA WAZEE
WILAYANI MBOZI WAMEPENDEKEZA KUSHIRIKISHWA WAKATI WA UHAMASISHAJI WA ZOEZI LA SENSA KUTOKANA NA UKWELI KWAMBA BADO KUNA
IMANI NA MILA POTOFU KWA JAMII WILAYANI
HUMO , HASA INAPOFIKIA HATUA YA KUHESABU
WATOTO KUWA NI UCHURO KWA KAYA ZAO.
AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA KAMPENI KWAAJILI YA HAMASA YA
SENSA WILAYANI HUMO, MWENYEKITI WA CCM WILAYA MBOZI MZEE ALOYCE MDALAVUMA,
AMESEMA NJIA PEKEE NI KWA WAZEE MAARUFU KUTUMIKA HASA MAENEO YA VIJIJINI KATIKA
KUTOA UFAFANUZI JUU YA UMUHIMU WA ZOEZI HILO ILI KUPATA MWITIKIO MKUBWA NA
KUWEZESHA MAFANIKO YA JUU YA ZOEZI LA SENSA
AMESEMA KWA JAMII YA WANYIHA KUHESABU WATOTO KATIKA HALI YA
KAWAIDA HAIKUBALIKI, LAKINI KWAKUWA ZOEZI LA SENSA LINAFAHAMIKA VYEMA UMUHIMU
WAKE NI VYEMA WANANCHI NA HASA WAZEE WAKAHAMASISHWA KUSHIRIKI VYEMA KWENYE
UHESABUJI ILI KUWEZESHA UPATIKANAJI WA
TAKWIMU SAHIHI
KWA UPANDE WAKE MZEE BENNY MWANG’AMBA AMESEMA KUNA HAJA KWA
VIONGOZI WA DINI WILAYANI HUMO KUTUMIA VITABU VITAKATIFU IKIWEMO BIBLIA AMBAPO
KUNA ENEO INAZUNGUMZIA MAJIRA AMBAYO YESU ALIZALIWA ULIKUWA WAKATI WA SENSA YA
WATU NA KWAMBA NJIA HIZO ZITAWEZESHA WATU KUFUNGUKA NA KUACHA USIRI KWENYE
TAARIFA ZA FAMILIA ZAO
MAPEMA KATIKA TAARIFA YAKE MRATIBU WA SENSA WILAYA YA MBOZI
BWANA ELIUD MWAKIBOMBAKI AMESEMA WILAYA YA MBOZI IMETEUA JUMLA YA MAKARANI 1471
WATAKAOSIMAMIA MAENEO YA UHESABUJI 230 AMBAPO MIONGONI MWAKE MAKARANI 460 WATAJIELEKEZA KATIKA DODOSO REFU
AMESEMA KATIKA MAANDALIZI YA ZOEZI HILO MAFUNZO YA
WAHESABUJI YANATARAJIWA KUANZA JULAI TISA KATIKA VITUO VINNE VYA VWAWA, IGAMBA,
ITAKA NA MAHENJE AMBAPO WAKUFUNZI WAMESHATENGWA KWA MAENEO HAYO ILI KUFANYA
MAANDALIZI YATAKAYOFANIKISHA ZOEZI HILO
AKIZINDUA ZOEZI HILO KWA KUPIGA KING’ORA MKUU WA WILAYA YA
MBOZI DR MICHAEL KADEGHE AMESEMA , PAMOJA NA KUANZISHA MASHINDANO YATAKAYOBEBA
UJUMBE WA SENSA KUANZIA NGAZI YA KIJIJI PIA WILAYA IMEJIPANGA KUHAKIKISHA KUWA
ZOEZI HILO LINAFANIKIWA NA HASA MAENEO YA VIJIJINI
DK KADEGE AMESEMA KATIKA KUFANIKISHA ZOEZI HILO WILAYA
IMESHATUMA TIMU YA UHAMASISHAJI AMBAPO PAMOJA NA MAMBO MENGINE TIMU HIYO
INAPOKEA CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA KUFANIKISHA ZOEZI HILO KUTOKA KWA
VIONGOZI WANGAZI ZA JUU NA WALE WA JAMII ILI HATIMAYE WAKATI WA UTEKELEZAJI
ZOEZI HILO LIWEZE KUWA LA MAFANIKIO