Adverts

Oct 8, 2012

SHIMIWI IKULU SPORTS YAWIKA NA KUTWAA VIKOMBE KIBAOMgeni Rasmi Katibu Mkuu Ikulu Bw Peter Ilomo Akikagua timu ya Ikulu sports club ya kamba wanaume aliyemwakilisha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue kwenye kilele cha mashindano ya Shimiwi mkoani Morogoro jumamosi tarehe 6.10 2012.
Timu ya Netball ya Ikulu sports club wakiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wao kabla ya fainali na timu ya Wizara ya Afya Ikulu sports club ilishida kwa magoli 50- 25 kuwa washindi wa kwanza.
Wachezaji wa Ikulu sports club na Wafanyakazi wenzao ambao walienda kushangilia timu yao wakifurahia baada ya kushinda na kupata vikombe vitano kwenye michezo ya Mpira wa pete, kamba wanaume, kamba wanawake, kuendesha baiskeli, na mshindi wa pili Riadha.
Ikulu sports club Kamba wanaume wakifurahia kikombe baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi.
Ikulu sports club yaongoza Yapata vikombe vitano kwenye mashindano ya Wizara na Taasisi za serikali (SHIMIWI) Mashidano hayo yalifanyika Mkoani Morogoro na kufungwa na Katibu Mkuu Ikulu Bw Peter Ilomo. 
KUTOKA MICHUZI BLOG