Adverts

Oct 12, 2012

UTAPELI WA KUTUMIA MAJINA YA VIONGOZI KWENYE M-PESA WAWAUMIZA WANANCHI

Wizi mpya ulioanza hivi sasa kwenye mifumo ya fedha ya kielektronikia ikiwemo MPESA, umewaliza wananchi wengi wilayani Mbozi ambapo jana jioni mmoja wa viongozi wa chama cha walimu alilizwa kiasi cha zaidi ya Milion Moja imefahamika.
Akizungumza wakati akifuatilia kwenye kituo kimojawapo kinachotoa huduma za MPESA katika mji wa Vwawa, kiongozi huyo wa kike alifikwa na tukio hilo baada ya kupigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni George Lubeleje ambaye ni Mbuge wa jimbo mojawapo la mkoa wa DODOMA akimtaka amsaidie kiasi cha shilingi 600,000 za mafuta wameishiwa wakiwa mikumi wakisafirisha maiti kwenda sumbawanga.
Inaelezwa kuwa kwakuwa anamfahamu, aliomba pia mwenyeji huyo amfanyie booking ya hoteli katika mji wa Vwawa ili ujumbe huo uweze kupumzika angalau usiku mmoja kabla ya kuendelea na safari ya kupeleka maiti Sumbawanga.
Mama huyo alifanya haraka kutoa fedha benki na kuzituma kwenye simu ya mheshimiwa huyo akijua ndiye Lubeleje halisi, na baada ya kutuma fedha hizo ripoti ya fedha kutumwa kwa njia ya MPesa ilionyesha kuwa jina ambalo fedha zimepokelewa ni George Lubeleje.
Hata hivyo dakika chache baada ya fedha kuingia kwenye simu hiyo, inaelezwa kuwa mh huyo feki alipiga simu tena kwa mwalimu huyo na kumweleza kuwa zimeingia lakini bahati mbaya tangu asajiri simu yake hajawahi kutumia huduma ya mpesa, hivyo alimwomba awapigie voda ili wazirejeshe fedha hizo na badala yake atumie simu ya dereva wake ambaye ana uzoefu wa kutumia huduma hizo za Mpesa.
Mwanamke huyo alisisitizwa kuwa angekopa mahala popote ili waweze kuondoka pale walipo waendelee na safari wakati yeye akiendelea kushughulikia kurejesha fedha hizo kutoka Vodacom, hata hivyo baada ya kutuma fedha hizo mara ya pili alienda kufuatilia kwenye kituo cha kutolea fedha lakini ikabainika kuwa fedha za awali zimechukuliwa.
Licha ya kuwasiliana na kampuni ya vodacom, majibu ya mtoa huduma hayakuonyesha kutii kiu ya mama huyo na kuamua kwenda kituo cha polisi cha Vwawa ili kutoa taarifa kuwezesha uchunguzi kufanyika kwakuwa inaonyesha kuwa mtandao huo umeingia kwa kasi wilayani mbozi na tayari watu wengi wamelizwa kutokana na aina hiyo ya utapeli.
Watu wanajiuliza imekuwaje watu wajisajiri kwa majina ya viongozi na mawaziri na makampuni ya simu yameendelea kukaa kimya bila kufuatilia taarifa za usajiri zinazofanywa hivi sasa na mawakala maarufu kama freelancers na kudanganywa na matapeli kutokana na uelewa mdogo walio nao baadhi yao.