Adverts

Jan 19, 2013

GARI LAPINDUKA NA KUUA NG'OMBE 25 PAPO HAPO, WANANCHI WACHANGAMKIA VIBUDU

Mama huyu akiwa eneo la Tukio kusubiria nyama ya bei chee iliyokuwa inauzwa na vijana waliojiajiri kuchinja  ng'ombe waliokufa kwenye ajali hiyo iliyotokea eneo la Old Vwawa wilayani Mbozi

Hapa jamaa akibeba kichwa cha ng'ombe baada ya kujimegea vipande vyake tayari kupeleka nyumbani

Hapa akipeleka nyumbani kwake kwa mwendo wa pole! vichwa viiwili mkononi e bwana eeee

Hapa maini yalishachambuliwa yamebakia mapupu huku ng'ombe huyu aliyehai akishuhudia wenzake wanavyocharangwa mautumbo yao mbele yake! ngombe huyu amevunjika miguu yote kwenye ajali hiyo

Hili ndilo gari lililotumbukia kwenye mto Old Vwawa na kuua ng'ombe 25 kati ya 46 waliokuwa wakisafirishwa kutoka sumbawanga kwenda mbeya,

Katika ajali hiyo ng'ombe mmoja kama anavyoonekana amening'inia kwenye bodi alishindwa kuchomolewa hapo, wakati huo pia watu watano wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo ambapo walitibiwa na kuruhusiwa

Afisa mifugo wilaya ya Mbozi bwana Thabit Rukarisha akizungumzia wananchi kuuziwa mizoga ya Ng'ombe ambao hawajapimwa katika miji ya Tunduma,VWAWA na Mlowo wilayani MboziPuch