Hii inapendekezwa kuwa ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Mbozi ambako DED ndimo atakamotumia
Afisa Utawala na Utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi bwana Lulandala alikuwa miongoni mwa wanaotembelea eneo la Momba kwaajili ya kuona mazingira hayo ya makazi ikiwa yataweza kufaa kwaajili ya maisha ya watumishi wanaohamishiwa huko
Padre Mande akizungumza na Uongozi wa halmashauri ya Momba kulia kabisa ni Mwenyekiti wa Halmashauri Bernard Sichilonga, akifuatiwa katikati Makamu Mwenyekiti Credo Simwinga na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Juma Kitabuge juu ya uwezekano wa kutumia jengo la Chekechea kwaaajili ya ofisi za idara mbalimbali za halmashauri hiyo ya Momba
Hapa ni Mjini Chitete ambako ndipo makao makuu ya wilaya ya Momba, wageni njoo wenyeji wapone nyuma ya Noaha jamaa akaamua kuuza kukuAfisa Utumishi Momba bwana Mfugale akaamua kutumia ziara hiyo kuweka kumbukumbu kwenye daraja la kitep tep ambayo kwa eneo hilo ni madaraja muhimu katka kurahisisha mawasiliano baina ya vijiji na vijiji
Wakiangalia shamba la ufuta katika moja ya vijiji vya kata ya chitete
Nyumba mojawapo ambamo watumishi wanatarajiwa kupangishwa baada ya kuanza maisha katika halmashauri ya wilaya ya Momba
MIUNDOMBINU kwaajili ya watumishi wanaohamia ni ya aina hii, watu wanajiuliza wataanza anza vipi?
Hapa ndipo sokoni kariakoo kwa wilaya ya Momba! namaanisha soko kuu la bidhaa mbalimbali kwaajili ya mahitaji ya nyumbani
haya ndiyo majengo yanayopendekezwa kutmiwa na halmashauri ya wilaya Momba kwaajili ya ofisi za idara mbalimbali ambayo awali yalijengwa kwaajili ya chekechea kupitia kanisa katoliki
PICHA ZOTE NA GODFREY MWAKITWANGE